KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 18, 2017

GODBLESS LEMA NA MKEWE KIZIMBANI TENA LEO

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Augustino Rwezile, leo, anatarajia kuwasomea hoja za awali Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na mkewe, Neema katika kesi inayowakabili ya kumtukana Mkuu wa mkoa huo, Mrisho Gambo. 

Hoja hizo ilikuwa wasomewe Novemba 15, 2016 lakini zilikwama kusomwa kutokana na Lema kuugua ghafla na Wakili wa Serikali, Elizabeth Swai kumuomba hakimu kutumia busara ya Mahakama kuisogeza mbele kesi hiyo kutokana na hali ya mbunge huyo. 

Lema bado anasota rumande kwa siku 76 tangu Novemba 2, mwaka jana baada ya kukosa dhamana katika kesi inayomkabili ya tuhuma za kutumia lugha ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli. 

Kutokana na sababu hiyo, Hakimu Rwezile pia aliahirisha kesi ya kuhamasisha maandamano ya Ukuta inayomkabili mbunge huyo na ile ya kumtumia ujumbe mfupi wa maneno Gambo unaodaiwa kuwa na matusi hadi leo. 

Katika kesi ya kuhamasisha maandamano inayomkabili Lema peke yake, shahidi ambaye ni Mkuu wa Makosa ya Jinai Mkoa (RCO) wa Arusha, George Katabazi ataanza kutoa ushahidi wake ambao ilikuwa atoe Novemba 15.

Awali, upande wa Jamhuri ulidai utakuwa na mashahidi watano katika kesi ya kuhamaisha maandamano na upelelezi umekamilika. 
Mashahidi wengine ni ASP Damas Masawe ambaye ni (OCCID), Inspekta Adam Nyamiti, WP 6826 DC Esta Yohana na Ezekiel Denis Kwayu kutoka kitengo cha Upelelezi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam. 

Kwa upande wa kesi ya Lema na mkewe ya kumtumia ujumbe wa matusi Gambo, itaanza kusomwa maelezo ya awali ambayo nayo itakuwa tayari kwa kuanza kusikiliza baada ya upelelezi kukamilika.

No comments:

Post a Comment