Na. Julius S. Mtatiro
Goodmorning. Katika
uchaguzi huu mdogo CUF ilikuwa inatetea kata 1 ya Kimwani Muleba na
CHADEMA ilikuwa inatetea kata 1 ya Duru, Babati. Kata zingine zote
zilikuwa za CCM na zilikuwa zinatetewa na CCM.
Matokeo yanaonesha
CCM imetetea viti vyake vyote vya udiwani (takribani 20), CUF
imenyang’anywa kiti chake kimoja (Kimwani) na CHADEMA imelinda kiti
chake kimoja (Duru).
Kwa vyovyote vile vyama mbadala haviwezi
kujivunia matokeo haya kwani havikuweza kuishinda CCM, na CCM haina cha
kutambia kwani imeongeza kata moja tu. Kwa sasa nina mambo kadha ya
kuzungumza;
- Hali halisi inaonesha kuwa kama vyama mbadala vingeshirikiana
vingelishinda kata si zaidi ya 7 hivi. Bahati mbaya mashirikiano haya
yalikosekana tangu mwanzo baada ya upande wa “CUF ya Msajili na Bwana
Yule” kusisitiza kuwa wataweka wagombea nchi nzima na hakuna UKAWA.
- Lakini pia, hata shajihisho la ushirikiano mkubwa zaidi lililokuja
kuzuliwa na kaka yangu Prof. Kitila Mkumbo lilifanywa TOO LATE kwa lengo
la kutafuta sababu ya kujificha baada ya matokeo. Niliwahi kusema,
kiuzoefu vyama haviwezi kuachiana maeneo wiki moja kabla ya siku ya
uchaguzi na kushauri hivyo si kwa nia njema.
- Baada ya CUF ya Msajili na Bwana Yule kujipanga kuvuruga uchaguzi
huu na kushusha spirit ya UKAWA, vyama vya NCCR na CHADEMA pia
vilionelea kila kimoja kijipiganie jambo ambalo ni kosa kubwa. Na
madhara ya migawanyiko yote yalijulikana.
- Uzoefu unaonesha kuwa, kuishinda CCM kwenye chaguzi ndogo ni nadra
mno. Kuliwahi kuwa na mfululizo wa chaguzi ndogo, Tarime, Busanda,
Tunduru, Mbeya Vijijini n.k. na kote huko CCM ilishinda isipokuwa Tarime
na baadaye Arumeru. Katika chaguzi ndogo CCM hutawanya rasilimali zake
nyingi zikajaa kwenye majimbo au kata hadi POMONI.
- Mkakati wa DOLA na CCM kuvitumia baadhi ya vyama au baadhi ya
viongozi kwenye vyama (mamluki) unaelekea kufanikiwa sana. Lakini, sera
za “Self Protectionism” ndani ya vyama mbadala hata kwenye mambo
yanayohitaji ushirikiano wa kitaifa zitaendelea kuvigharimu vyama vyetu.
- Good News kwa ACT Wazalendo kwamba huenda ndicho chama
kilichofanikiwa kwenye uchaguzi huu kuliko vyama vyote (CCM inclusive)
kwani pamoja na uchanga wake kimevishinda baadhi ya vyama vikongwe
kwenye kata chache (kwa idadi ya kura na si ushindi wa jumla). Na hiyo
ni alert call kwamba ACT is needed in the UKAWA basket na kwa hiyo ianze
ku BEHAVE like a true party wakati UKAWA pia ikiiandalia mazingira
kisaikolojia.
- Bado CCM inashinda chaguzi kwa kutumia mifumo ilele; rushwa, mabavu,
hila, wawakilishi wa NEC na NEC yenyewe, uwezo wa uelewa wa wapiga kura
(Mfano. CCM imepeleka uandikishaji wa Bima ya Afya kwa wananchi kata ya
Nkome, wakati wa uchaguzi = Rushwa).
- Vyama vya upinzani vinashindwa chaguzi hizi kwa sababu ya kukosa
ushirikiano wa kweli baina ya vyama hivyo, maelezo namba 7 hapo juu na
sentensi ya kwanza ya maelezo yaliyo namba 5 hapo juu.
- Kwa hakika, matokeo haya hayana athari zozote za kufaulu kwa
Magufuli katika sera zake au kushindwa kwa Magufuli katika sera zake.
Yaani, CCM ya Magufuli haijawa na ushawishi wa ziada kwa wapiga kura ili
kupata ushindi huu kwenye ngome zake. CCM bado inashinda chaguzi kibabe
na kwa mkakati dola zaidi bila kujali nani yuko madarakani.
- Sijaona connection yoyote kati ya matokeo haya na siasa za 2020.
Vyama vyote vinayo fursa ya kuendelea kujipanga na kama tutafanikiwa
kuuvunja mfumo dola unaoathiri vyombo vya uchaguzi na uhuru wake,
unaoondoa mazingira sawa kwa vyama kufanya siasa n.k, mabadiliko ya
kikatiba kwenye NEC na sheria za uchaguzi na mengine mengi, siasa za
2020 zitakuwa mbichi sana.
|
No comments:
Post a Comment