![]() |
Msiba
wa mama mdogo wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, umewakutanisha kwa mara
ya kwanza hadharani kiongozi huyo wa Serikali ya awamu ya nne,
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe
na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bernard Membe.
Wakati
wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, viongozi hao walionekana mahasimu zaidi
baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, jina lake kukatwa
katika kinyang’anyiro cha mbio za urais ndani ya CCM na kuhamia Chadema.
Baada
ya Uchaguzi Mkuu kumalizika, Rais huyo mstaafu hakuwahi kuonekana
hadharani akiwa na viongozi hao wa upinzani, huku Membe yeye akiwa
haonekani kabisa kwenye mambo ya siasa wala mikusanyiko yoyote ile.
Lakini
jana mazishi ya mama huyo, Nuru Khalfan, mbali ya kuwakutanisha
viongozi hao, yaliwakutanisha pia Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda na
Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Nape Nnauye.
Wengine walioudhuria ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo.
Waziri mkuu, Kassim Majaliwa, ndiye aliyeongoza mamia ya waombolezaji kwenye mazishi hayo yaliyofanyika Bagamoyo mkoani Pwani.
Mara
baada ya kumalizika kwa mazishi hayo, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani
Kikwete, aliwashukuru wananchi wote waliojitokeza kushirikiana nao
kwenye msiba huo.
Alisema madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Muhimbili wamefanya kazi kubwa katika kipindi alichokuwa bibi yake amelazwa.
"Naomba
niwashukuru madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH) kwa sababu wamefanya kazi kubwa sana katika kipindi chote ambacho
mgonjwa amelazwa hadi alipofariki," alisema Ridhiwani.
|
March 9, 2017
MBOWE ALIVYOSHIRIKI MSIBA WA MAMA MDOGO WA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment