![]() |
Baada
ya Askofu Josephat Gwajima kutumia zaidi ya wiki tatu kuzungumzia suala
la dawa za kulevya na elimu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda kwa madai kuwa ametumia cheti cha mtu, ndugu yake kiongozi huyo
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ameibuka na kumshambulia akimtaka aache
mamlaka husika zifanye kazi yake.
Mwanasheria
Methusela Gwajima ambaye ni mdogo wake Askofu Gwajima akizungumza na
waandishi wa habari leo amehoji, kwanini suala la elimu ya Makonda
limeibuliwa wakati huu ambapo amevalia njuga suala la vita dhidi ya dawa
za kulevya.
"Watu
hawa wanaozungumzia elimu ya Makonda walikuwa wapi? Tangu akiwa Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni hawakusema chochote ila amegusa dawa za kulevya
ndio wameibuka na kuanza kumshambulia?"
Methusela amesema hamaanishi kuwa mabaya ya Makonda yasinguzumzwe, lakini kwanini yamekuja wakati huu?
"Kwanini wanataka kutuhamisha kwenye ajenda yetu iliyopo mezani?. Yani sasa Watanzania tumehamishwa tukaacha kujadili suala la dawa za kulevya na kwenda kujadili cheti cha mtu. amesema Methusela.
Mwanasheria
huyo ametahadharisha kuwa kama vita hii dhidi ya dawa za kulevya
itashindwa, huenda asiibuke mtu mwingine mwenye ujasiri kama Makonda kwa
sababu kila mmoja atakuwa anahofia kufanyiwa kama alivyofanyiwa
Makonda. Na haya yatakapotokea basi wahusika wa biashara ya dawa za
kulevya ndio watakuwa wameshinda.
Wakati
huo huo, amemshambulia kaka yake kwa kugeuza suala la dawa za kulevya
na elimu ya makonda kuwa sehemu ya mahubiri kanisani kwake.
“Wewe
umeshatuhumiwa, umeitwa Polisi, hivi kwanini usisubiri uchunguzwe? Kama
wewe huhusiki si utaambiwa basi. Wameitwa watu wengi, wameitikia wito,
kwanini sasa yeye amegeuza kuwa ajenda? Mbaya zaidi imekuwa ni ajenda
kanisani. Kwa hiyo kanisa limegeuzwa kuwa kijiwe cha siasa na watanzania
wamekaa kimya hawasemi,” alieleza Methusela
"Kama
Gwajima anadhani kuwa ameonewa aende mahakamani badala ya kukaa na
kulalamika. Kwanini basi anakwepa mahakama na kufanya kanisa ndio sehemu
ya kuzungumzia, kila Jumapili ni Makonda, Makonda, Makonda, vyeti,
vyeti" amehoji Methusela.
Mwanasheria
Methusela amesema ni lazima watanzania wajiulize ni kundi gani lililopo
nyuma ya Askofu Gwajima ambalo ndilo linamsukuma kuendelea kumshambulia
Mkuu wa Mkoa na kusababisha kuachwa kwa ajenda ya msingi.
|
March 9, 2017
MDOGO WAKE ASKOFU GWAJIMA AIBUKA NA KUMSHAMBULIA KAKA YAKE KWA KUTAKA VYETI VYA MAKONDA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment