Mkuu wa Wilaya ya Chemba Ndugu Simon Ezekiel Odunga akizungumza na wananchi wa kata ya Farkwa wakati wa uzinduzi wa zoezi la uthamini mali ili kupisha ujenzi wa bwawa la Farkwa. |
Mkuu
wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma akiongozana na baadhi wa Viongozi wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Chemba, Wataalamu wa Halmashauri, Wataalamu kutoka Wizara ya Maji, Uvuvi
na umwaguliaji, Wataalamu wa Bonde la Kati na Wataalamu kutoka Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wamezindua zoezi la uthamini wa mali za wananchi wa
vijiji viwili vya Mombose na Bubutole watakaohama kupisha mradi mkubwa
wa Ujenzi wa bwawa la Farkwa mkoani hapa.
Mradi wa bwawa la Farkwa ni mradi
mkubwa ambao huenda ukawa ni mkubwa katika Ujenzi wa mabwawa makubwa
kuliko yote barani Afrika. Mradi huu uliasisiwa na baba wa Taifa tangu
mwaka 1970 utazinufaisha Wilaya za Bahi, Chemba, Chamwino na Dodoma
Manispaa na utegemea kutumia pesa za Tanzania zaidi ya Tilioni 2.
Kufuatia umuhimu wa mradi huu na
uwijio wa makao makuu ya nchi mkoani Dodoma, serikali imezamilia ifikapo
mei mwaka huu zoezi la Uthamini wa mali za wananchi wanaohama kupisha
mradi huu mkubwa katika Vijijini vya Mombose na Bubutole vilivyopo
Wilayani Chemba pamoja na vijiji vinavyopitiwa na njia Kuu ya bomba
linalopeleka Maji eneo la Kilimani mjini Dodoma liwe limekamilika tayari
kwa kuwalipa wananchi ili Ujenzi wa bwawa uanze.
Ujenzi wa mradi huu unategemea
kuchukua miaka mitatu 2017-2021 mpaka kukamilika kwake. Hivyo wananchi
wametakiwa kutoa ushirikiano kwa Wataalamu wa uthamini kwa kuwa
wameusubiri mradi huu kwa zaidi ya miaka 47 na leo serikali imepata
fedha ya kuutekeleza.
Mhe Mkuu wa Wilaya ya Chemba Ndugu
Simon Odunga wamewataka wananchi hao kujiepusha na watu wasiopenda
maendeleo yao na nchi yetu kwa ujumla wa anaopita pita huko na kujifanya
watetezi wa haki za wananchi. Swali hao watetezi walikuwa wapi tangu
1970 waje leo ambapo mradi unaanza kutekelezwa.?
Aidha, amesisitiza wananchi ambao
ni wamiliki halali wa maeneo husika ndio wajitokeze kwenye uthamini huo
ili kuepusha udanganyifu na migogoro isiyo ya lazima wakati wa malipo
yatakopoanza. Kwani kuna baadhi ya wananchi zi waaminifu na atakayefanya
hivyo akibaini sheria kali dhidi yake zitachukua mkondo.
Kwa upande wa Wataalamu Mkuu huyo
wa Wilaya amewataka kutumia akili, uweledi na taaluma zao katika
kuhakikisha kila mwananchi wa maeneo hayo anapata haki yake stahiki kwa
mujibu wa sheria za uthamini.
Katika Mkutano huo Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Mhe Rajabu Muheshimwa ameongea kwa
kupongeza juhudi za Serikali kwa kuamua kuanza mradi huu na zaidi kusihi
wananchi kutoa ushirikiano kwa Wataalamu, hali kadhalika Mhe Diwani wa
Kata ya Farkwa Ndugu, Suleiman Gawa amesisitiza kuhakikisha wananchi
wanashiriki kikamilifu pia Wataalamu wahakikishe wanaorodhesha mali zote
za wananchi zinazotambulika kisheria ili kuepusha migongano hapo
baadae.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya
amewataka Viongozi wa Vijiji na vitongoji kusimamia zoezi hili
kikamilifu kwani wao ndio wanaowafahamu wananchi wao pia watoto ambao
wanamiliki mali lakini hawatambuliwi kisheria kutokana na umri wao.
|
No comments:
Post a Comment