![]() |
Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na
Usimamizi wa Ligi za Tanzania (Kamati ya Saa 72), imemwondoa Mwamuzi wa
kati, Ahmada Simba katika orodha wa waamuzi watakaochezesha mechi za
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu wa 2016/2017.
Hatua hii imefikiwa baada ya
utetezi wa Mwamuzi Simba kudai kwamba hakuona tukio la Mchezaji wa Young
African, Obrey Chirwa ambaye alifunga bao ambalo hata hivyo, mwamuzi
alilikataa na kumwonya mchezaji kwa kadi njano.
Tukio hilo lilitokea katika mchezo
ambao Young Africans walikuwa wageni wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa
Taifa, Machi mosi, mwaka huu.
Katika hiyo ya njano ilikuwa ni ya
kwanza kwa Chirwa ambayo hata hivyo kamati ya Saa 72 imeifuta kadi hiyo
kwa mujibu wa kanuni ya 9 (8) baada ya Kamati ya Saa 72 haikupaswa
kutolewa kwa Chirwa kwa sababu hakukuwa na kosa wala mazingira ya
kuonywa.
Kadi hiyo ilikuwa ni msingi wa
kadi nyekundu baada ya Chirwa kufanya faulo ambayo aliadhibiwa tena kwa
kadi ya njano hivyo kutolewa nje kwa mujibu wa taratibu.
Kufutwa kwa kadi ya njano ya
kwanza, kunapelekea kufutwa kwa kadi nyekundu ambayo msingi wa kadi hiyo
ulisababisha kadi nyekundu hivyo mchezaji angempaswa kukosa mchezo
mmoja. Hata hivyo, kadi ya pili ya njano inahesabiwa.
Kadhalika uamuzi mwingine ulikuwa
ni kuipiga faini Young Africans iliyocheza na Simba Februari 25, 2017
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya Wanajwani hao
kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.
Kitendo hicho ni kwenda kinyume
cha kanuni ya 14 (14) ya Ligi Kuu inayoelekeza kuwa timu zitaingia
uwanjani kwa kutumia milango rasmi. Hivyo kwa kuzingatia Kanuni ya 14
(48) ya Ligi Kuu, Kamati imeipiga Young Africans fainali ya Sh 500,000
(lakini tano).
|
March 9, 2017
MWAMUZI ALIYEKATAA BAO LA CHIRWA AONDOLEWA LIGI KUU YA VODACOM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment