MWENYEKITI wa chama cha
mapinduzi (CCM) tawi la Mparange na mjumbe wa serikali ya kijiji cha
Ikwiriri Kaskazini ,wilayani Rufiji mkoani Pwani, Michael
Lukanda,ameuawa kwa kupigwa risasi ya kichwani na watu wasiojulikana.
Watu hao wanadaiwa kuwa
ni wawili waliotumia usafiri wa pikipiki ambapo mmoja walimpiga risasi
marehemu mlangoni akiwa anataka kuingia nyumbani kwake kisha
walitokomea.
Tukio hilo limefuatia
baada ya mwenyekiti wa kitongoji cha Mparange kijijini hapo, Bakari
Mpanawe kunusurika kifo baada ya kupigwa risasi ya tumboni na mkononi
march 19.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani ,Onesmo Lyanga ,alikiri kutokea kwa tukio hilo usiku wa kuamkia march 29.
Alisema tukio hilo ni la tano kutokea ndani ya mwezi huu ,likihusisha uhalifu wa kutumia silaha za moto .
Kamanda Lyanga ,alieleza
kwamba wanaendelea kuwasaka watu waliohusika kufanya matukio hayo ili
waweze kuchukuliwa hatua za kisheria .
Kwa upande wake ,katibu
wa CCM wilayani Kibiti, Zena Mgaya ,alisema hali ya kiusalama sio
shwari katika baadhi ya maeneo wilaya ya Kibiti na Rufiji kijumla.
Alisema hali hiyo inajenga hofu kwa viongozi kupitia CCM ambao baadhi yao wameamua kukimbia miji kwa kuhofia kuuawa .
Zena alibainisha
kwamba,matukio ya aina hiyo yanawasababishia kuishi pasipo na amani na
wanaccm kuhofia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi
zijazo za chama na serikali za vijiji na vitongoji.
Alihamasisha wanaccm kugombea nafasi mbalimbali bila kuweka uoga kwani kifo kinapangwa na mungu .
Nae diwani wa kata ya
Dimani ,Ramadhani Manyema ,alisema kuna wenyeviti wa vitongoji na vijiji
vinne wamekimbia miji yao wakihofia maisha yao .
Alisema kukimbia maeneo
yao ya kazi kumetokana na kutokea matukio ya hivi karibuni ambapo kuna
Mwenyekiti wa kijiji cha Nyambonda pamoja na wenyeviti wa vitongoji
viwili na mtendaji wa kijiji hicho kupigwa risasi .
Maeneo mengine ni Jaribu
Mpaka ambako OC CID na mgambo wa maliasili walipigwa risasi na
kufariki na huko eneo la Kifugo tendaji alijeruhiwa kwa kupigwa risasi .
Manyema alieleza ,hali ya kiusalama sio shwari hivyo wanatilia mashaka kama watafanikiwa katika zoezi la uchaguzi wa chama .
Aliliomba jeshi la polisi mkoani Pwani ,lishuke vijijini ambapo hali sio nzuri pasipo kukaa mjini pekee .
Akizungumza katika ziara
yake wilayani Kibiti,katibu wa CCM mkoani Pwani, Hassan Mtenga
aliwataka wazazi na walezi kuwafuatilia nyendo watoto wao kwani wapo
vijana wanaotumika kwenye matukio ya kiuhalifu .
Mtenga alisema ifikie hatua ya watu kubadilika kwa kuacha kuficha wahalifu kisa ni ndugu ,jamaa ama marafiki .
|
March 30, 2017
MWENYEKITI WA CCM TAWI LA MPARANGE RUFIJI APIGWA RISASI NA KUFARIKI DUNIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment