KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

March 25, 2017

SAMATTA AING’ARISHA TAIFA STARS DHIDI YA BOTSWANA,APIGA GOLI MBILI

1
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kilichocheza na timu ya taifa ya Botswana leo kwenye uwanja wa Taifa kikiongozwa na mchezaji wa kulipwa anayechezea timu ya Genk ya Ubelgiji Mbwana Samata.
2
Waziri wa Habri, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na wachezaji wa timu ya taifa ya Botswana kabla ya mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa leo.
3
Waziri wa Habri, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Sytars kabla ya kuchezwa kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
……………………………………………………………………………………
Mshambuliaji wa Kimataifa na pia hucheza Ligi Kuu ya Ubelgiji Mbwana Ally Samatta ameisaidia Taifa Stars kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Botswana huku yeye akifunga magoli yote mawili mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Na ulikuwa mchezo wa kwanza Taifa Stars inacheza chini ya kocha wake mpya, Salum Mayanga aliyerithi mikoba ya Charles Boniface Mkwasa aliyeng’atuka Janauri. Katika mchezo huo uliodhuhuriwa na Waziri mpya wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, DK Harison Mwakyembe, ilimchukua dakika mbili tu mshambuliaji huyo wa KRC Genk ya Ubelgiji kuwainua vitini wapenzi wa soka wa Tanzania waliojitokeza kuangalia Mpira huo akimalizia pasi ya beki Mohamed Hussein Tshabalala na kumtoka beki Kaone Vanderwesthuizem kabla ya kumchambua kipa, Kabelo Dambe.
Baada ya bao hilo, Botswana wakabadilisha aina ya uchezaji na kuacha kujilinda zaidi na badala yake kuanza kupeleka mashambulizi langoni mwa Stars. Hali hiyo iliitia misukosuko kidogo ngome ya Taifa Stars, lakini siofa zimuendee kipa Aishi Salum Manula aliyeokoa hatari zote.  Kipindi cha pili, mchezo uliendelea kuwa wa kushambuliana kwa zamu, ingawa Stars ndiyo wal8oendelea kung’ara zaidi uwanjani. Wafungaji hodari katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Shiza Kichuya wa Simba SC na Simon Msuva wa Yanga haikuwa bahati yao leo, kwani walipoteza nafasi kadhaa nzuri za kufunga. Winga Farid Mussa wa Tenerife ya Hispania alimkatia pasi nzuri Nahodha Samatta na wakati analielekea lango la Botswana akaangushwa na Thero Setsile nje kidogo ya boksi. Samatta akaenda mwenyewe kupiga shuti la mpira wa adhabu kiufundi na kuifungia bao la pili Taifa Stars dakika ya 87. Kikosi cha Tanzania kilikuwa: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Abdi Banda, Himid Mao/Jonas Mkude, Simon Msuva/Said Ndemla, Frank Domayo/Muzamil Yassin, Mbwana Samatta, Ibrahim Hajib na Shiza Kichuya/Farid Mussa.  Botswana: Kabelo Dambe, Tapiwa Gadibolae, Kaone Vanderwesthuizem, Lesenya  Ramoraka, Lesego Galenamotlhale, Ofentse Nato, Lebogang Ditsele, Omaaatla Kebatho, Mosha Gaolaolwe, Thacng Sesenyi na Mogakolod Ngele

No comments:

Post a Comment