KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

March 26, 2017

TANESCO YATOA TAARIFA YA KATIZO LA UMEME SEHEMU KUBWA YA JIJI MACHI 26



logo-tanesco
SHIRIKA  la Umeme Tanzania (TANESCO), limesema kituo kikubwa cha kupoza na kusambaza
 umeme cha Ilala jijini Dar es Salaam, kitakuwa kwenye maboresho makubwa Machi
 26, 2017 na hivyo itapelekea eneo kubwa la jiji la Dar es Salaam kukosa umeme.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO makao makuu, Bi. Leila Muhaji
 imesema umeme utakosekana kuanzia saa 3 asubuhi na kurejea saa 10 jioni ambapo
 ametaja maeneo yatakayoathirika kufuatia kazi ya kuboresha kituo hicho ni
 pamoja na eneo la katikati ya jiji, Upanga, Kariakoo, Buguruni, Ilala, Mbagala
 na Chang’ombe.

Aliyataja  maeneo mengine kuwa ni pamoja na Kurasini, Kiwanda cha saruji Maweni, Wizara ya
 Maliasili na Utalii, (Mpingo House),Tusiime Mission na Tanzania Oxygen. Mengine
 yaliyotajwa ni pamoja na Ofisi ya Manispaa ya Temeke, Unilever, Mkuu wa Wilaya
 ya Temeke, Uwanja wa Taifa, Makao Makuu ya Puma, Temesa, Jarmana Printers,
 Quality Plaza, Notco, Bima ya Afya, Bandari Gate, na maeneo jirani.

Bi.  Leila aliyataja maeneo mengine kuwa ni pamoja na Goldstar, Quaim, Robbarac,
 Simba Plastic, Veta, Duce, JKT Mgulani Barracks,  Keko, Mkuranga,Chuo cha Diplomasia, 21st
 Century, Oilcom, Engen na eneo la Mtoni Mtongani.

Aidha kufuatia katizo hilo la umeme, TANESCO imetoa tahadhari kwa wananchikutoshika
 nyaya za umeme zilizokatika na kwuataka watoe taarifa kwenye namba za dharura
 za TANESCO.

Leila  alisema, uongozi wa TANESCO unaomba radhi kutokana na usumbufu utakaojitokeza
 kutokana na kazi hiyo.

No comments:

Post a Comment