Wawakilishi wa Tanzania katika
Michuano ya Klabu bingwa ya Afrika Yanga wamejiweka katika hali mbaya
ya kusonga mbele baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na
Zanaco ya Zambia katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 32 bora katika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matokeo yanamaanisha Yanga watahitaji ushindi wa ugenini katika
mchezo wa marudiano nchini Zambia ili kuingia hatua ya makundi ya
michuano hiyo.
Simon Msuva aliifungia Yanga
dakika ya 39 akimalizia pasi nzuri ya Mzambia Justine Zulu hadi
mapumziko wenyeji walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili Zanaco walikuja na mbinu mapya na kufanikiwa
kuziba mianya ya Yanga kupasiana pasi hivyo kuweza kutawaala eneo la
kiungo cha kati na kuwafanya vijana wa Lwandamina kushindwa kutawala
katikati.
Mshambuliaji wa kulipwa kutoka
nchini Ghana Attram Kwame aliisawazishia Zanaco dakika ya 78 kutokana na
Mpira uliochezwa kwenye eneo la 18 la Yanga na kumkuta mfungaji akiwa
kwenye nafasi ya kufunga huku akiwa peke yake na kumchambua mlinda
mlango wa Yanga Dida.
Hadi Mpira unamalizika Yanga
wameweza kugawana pointi na Wazambia hao na kujiweka katika wakati Mgumu
wa kutinga kwenye hatua ya makundi huku wakihitaji ushindi zaidi katika
mchezo wa marudiano utakaochezwa Machi 17 au 18 mwaka huu mjini Lusaka
ZambiaVIKOSI: Deogratius Munishi ‘Dida’, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vincent Bossou, Kevin Yondan, Simon Msuva, Justin Zulu, Donald Ngoma/Emmanuel Martin dk58, Thabani kamusoko/Juma Mahadhi dk60 na Obrey Chirwa.
Zanaco; Racha Kola, Ziyo Kola, Zimiseleni Moyo, Chongo Chirwa, Saith Sakala/Kennedy Musonda dk69, Taonga Mbwemya, Richard Kasonde, Attram Kwame, Augustine Mulenga, Ernest Mbewe na George Chilufya
No comments:
Post a Comment