KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 25, 2017

AJINYONGA HADI KUFA MWANZA

****Mtu mmoja amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya katani wilayani nyamagana.

****Mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kupatikana akiwa na pombe iliyohifadhiwa kwenye vifungashio vya plastiki almaarufu viroba pakiti 103 wilayani ilemela.

Kwamba tarehe 23.04.2017 majira ya 18:45hrs jioni katika mtaa wa mkuyuni sokoni kata ya mkuyuni wilaya ya nyamagana jiji na mkoa wa mwanza, mtu mmoja mwanamume aliyrfahamika kwa jina la faraja anselem miaka 31, mkazi wa mtaa wa mkuyuni sokoni, alikutwa akiwa amejinyonga chumbani kwake hadi kufariki dunia kwa kutumia kamba ya katani aliyokua ameifunga kwenye paa la chumba, kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Inasemekana kuwa taraehe tajwa hapo juu marehemu alibaki mwenyewe nyumbani, aidha inadaiwa kuwa kabla ya kufanya tukio hilo marehemu alionekana akiingia chumbani kwake kisha akafunga mlango ndipo baada ya muda kupita watoto waliokua wakicheza maeneo hayo waliona miguu ikining’inia dirishani ndipo walitoa taarifa kwa wazazi wao.

Majirani baada ya kuona tukio hilo walitoa taarifa polisi, ambapo askari walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kuukuta mwili wa marehemu ukining’inia mahali hapo, mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya bugando kwa ajili ya uchunguzi pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi. Aidha upelezi kuhusiana na kifo hicho bado unaendelea.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishina wa polisi ahmed msangi anatoa wito kwa wakazi wa jiji na mkoa wa mwanza, akiwaomba kuwa pale watakapoona mtu amekuwa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu hadi inapelekea kuweza kufanya kitu kisicho cha kawaida cha kuweza kujidhuru yeye mwenyewe au watu wengine, wamfikishe kwa wataalamu wa ushauri nasaha ili waweze kumshauri na kumwaondoa katika hali hiyo ya msongo wa mawazo na kisha kurudi katika hali ya kawaida na kuweza kuendelea na maisha.

Katika tukio la pili,
Kwamba tarehe 23.04.2017 majira ya saa 14:33hrs katika mtaa wa kiloleli kata ya nyamanoro wilaya ya ilemela jiji na mkoa wa mwanza, askari wakiwa doria na misako walifanikiwa kumkamata mtu aliyefahamika kwa jina la donatus sebastina miaka 16, mkazi wa kiloleli akiwa na pombe iliyeowekwa kwenye vifunganishio vya plastiki almaarufu viroba aina ya empire pakiti 103, kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Awali askari wakiwa kwenye doria na misako walipokea taarifa kutoka kwa wasiri kwamba maeneo tajwa hapo juu yupo mtu anayefanya biashara ya kuuza pombe ya viroba kwa siri, kutokana na taarifa hizo askari walifanya upelelezi wa kimyakimya huku wakiendelea na doria ndipo baada ya muda waliweza kufahamu mahali anapoishi mtuhumiwa na kufanikiwa kumkamata akaiwa na pakiti 103 za pombe iliyohifadhiwa kwenye vifungashio vya plastiki almaarufu viroba aina ya empire.

Mtuhumiwa yupo katika mahojiano na polisi, pindi uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakani, aidha upeleezi na misako ya kuwatafuta watu wengine wanaojihusisha na biashara hiyo ya pombe za viroba bado unaendelea.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishina wa polisi ahmed msangi anatoa wito kwa wakazi wa jiji na mkoa wa mwanza akiwataka kuendelea kutoa taarifa mapema kwa jeshi la polisi ili watu wanaojihusisha na biashari hiyo ya pombe za viroba waweze kukamatwa na kifikishwa katika vyombo vya sheria.

Imetolewa na:
Dcp: Ahmed Msangi.
Kamanda wa Polisi (m) Mwanza

No comments:

Post a Comment