MHUBIRI
wa Kanisa la IEACT lililoko Manispaa ya Shinyanga, Eliamani Kisanaga,
amebubujikwa na machozi kutokana na vitendo vya kinyama vinavyoendelea
hapa nchini vya kuuawa kwa polisi.
Kutokana
na hali hiyo, aliwashauri Watanzania kumrudia Mungu kwa kuishi kwa
kupendana kama alivyoagiza katika vitabu vitakatifu. Mhubiri huyo
alitokwa na machozi wakati wa Misa ya Pasaka, iliyofanyika juzi, kwenye
kanisa hilo. Pia alitumia fursa hiyo kuwaaga waumini wa kanisa hilo kuwa anahama.
"Tuishi kama Kristu kwa kuiga matendo yake, tusijiite Wakristu tu bila matendo, huko ni kujidanganya kwani hakuna kitabu kinachohubiri kuua, hiyo ni njia ya shetani. Tunakokwenda Watanzania wenzagu ni kwenye laana," alisema.
Aliongeza:
"Nchi yetu katika sura ya kimataifa, tulikuwa na sura nzuri ya amani na
upendo, lakini ghafla yakaanza mauaji ya vikongwe, mauaji ya walemavu
wa ngozi, dawa za kulevya na leo tunaua askari wetu wanaotulinda,
tunakwenda wapi?"
Pia, aliwataka Wakristo kuishimaisha mema na kuwa mfano kwa watu wengine ambao si wakristo
Pia, aliwataka Wakristo kuishimaisha mema na kuwa mfano kwa watu wengine ambao si wakristo
No comments:
Post a Comment