KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 30, 2017

HISA ZA ACACIA ZASHUKA SOKO LA HISA

Kupungua kwa bei za hisa za kampuni ya ACACIA kwa asilimia 32.7, na UCHUMI 28.6% na JHL 17.8% kumetajwa kuwa sababu ya kupungua kwa ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa Sh. Trilioni 1.5 kutoka Shilingi Trilioni 19.9 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 18.4 wiki iliyoishia tarehe 26 Mei 2017.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Miradi na Masoko wa DSE Patrick Mususa, pia alisema mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia Mei 26, 2017 yamepungua kutoka thamani ya Sh. Bilioni 29.5 wiki iliyopita hadi Shilingi Bilioni 2.9, kutokana na mauzo ya hati fungani 7 za serikali zenye thamani ya bilioni 3.8 kwa jumla ya gharama ya bilioni 2.9.

kwa upande wa viashiria,Mususa alisema “Kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepungua kwa pointi 171 kutoka pointi 2,288 hadi pointi 2,117 kutokana na kupungua kwa bei za hisa za kampuni mbali mbali zilizopo sokoni. Wakati Kiashiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimeongezeka kwa pointi 6 kutoka pointi 3,357 wiki iliyopita hadi pointi 3,363 wiki hii.”

“Sekta ya viwanda imeendelea kubaki kwenye pointi 4,228 wiki hii. Sekta ya huduma za kibenki na kifedha  wiki hii imeongezeka kwa pointi 17 kutoka pointi 2,551 hadi pointi 2,568 kutokana na kuongezeka kwa bei ya hisa za CRDB kwa asilimia 2.7%.Sekta ya huduma za kibiashara wiki hii imeendelea kubaki kwenye pointi 2,969,” alisema.

Pia, Mususa alisema thamani ya mauzo ya hisa imepungua kutoka Sh. Bilioni 8 wiki iliyopita hadi Shilingi Bilioni 2.6 wiki hii.

Hata hivyo, Mususa alieleza kuwa, idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imeongezeka kutoka hisa Milioni 1.1 hadi hisa Milioni 2.2, hali kadhalika mtaji wa kampuni za ndani umeongezeka kwa Bilioni 13 kutoka Shilingi Trilioni 7.056 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 7.069 wiki hii. kutokana na kuongezeka kwa bei ya hisa za CRDB (2.7%)

No comments:

Post a Comment