KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 19, 2017

MAJERUHI ARUSHA: HABARI ZAIDI KUHUSU MTOTO DOREEN BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI JANA.

Taarifa mpya za usiku huu kuhusu hali ya  Mtoto Doreen ( kwa mujibu wa mbunge Lazaro Nyarandu)   ni kuwa amemaliza kufanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo na Madaktari wamesema wamefanikiwa kwa ufanisi mkubwa kupita matarajio.

Doreen alikuwa afanyiwe upasuaji kwa makadrio ya masaa matano na dakika 30 lakini zoezi hilo lilikamilika kwa masaa manne huku timu ya “Surgical Support” IKIWA na watu 6 na wakiongozwa na Madaktari bingwa wawili, Dr. Meyer na Dr. Durward.

Mtoto Doreen amehamishwa kutoka chumba cha upasuaji na kupekewa ICU na Madaktari wamesema kwasababu hali yake imeridhisha sana, baadae leo watamtoa ICU ambako wamempumzisha baada ya upasuaji na kumrudisha wodi ya watoto

No comments:

Post a Comment