Rais wa Marekani Donald Trump
anazuru Israel na Maeneo ya Wapalestina leo, akiendelea na ziara yake ya
kikazi katika maeneo ya Mashariki ya Kati.
Atafika maeneo hayo
akitokea Saudi Arabia, mshirika muhimu wa Marekani, ambako alitoa hotuba
katika mkutano mkuu wa nchi za Kiarabu na Kiislamu.Bw Trump anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Israel na Palestina katika kipindi cha siku mbili atakazokuwa eneo hilo.
Rais huyo amesema kupatikana kwa mkataba wa amani kati ya Waisraeli na Wapalestina yatakuwa mafanikio makubwa, lakini hakusema mkataba kama huo unafaa kuchukua mwelekeo gani.
Amesema angependa sana pande zote mbili ziamue kuhusu mkataba huo wa amana kwa mashauriano ya moja kwa moja.
Katika mkutano mkuu wa viongozi wa Kiislamu na Kiarabu mjini Rihadh siku ya Jumapili, Bw Trump aliwataka viongozi hao kuwa kwenye mstari wa mbele katika kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu na wapiganaji wenye itikadi kali na "kuwafurusha kutoka kwenye dunia hii."


No comments:
Post a Comment