KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 25, 2017

NYAMLANI AJITOA KUWANIA URAIS TFF

index
Makamu wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani amejitoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.
Nyamlani aliwasilisha barua TFF leo Jumapili Juni 25, mwaka huu ikiwa ni siku moja tu tangu Kamati ya Uchaguzi ipitishe jina lake kuwa miongoni mwa wagombea 10 wanaowania nafasi hiyo ya urais. Sababu aliyoeleza ni masuala binafsi.
Kwa msingi huo, wagombea wanaobaki kwenye kinyang’anyiro na kuhitajika kufika kwenye usaili kuanzia Juni 29, mwaka huu ni tisa wakiongozwa na Rais wa sasa, Jamal Malinzi anayetetea nafasi.
Mbali ya Malinzi wengine wanaowania nafasi hiyo ni Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Fredrick Mwakalebela, John Kijumbe, Shija Richard, Ally Mayay na Emmanuel Kimbe.
Waliojitokeza kuwania Makamu wa Rais na kurejesha fomu wako Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Geofrey Nyange, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa.
Mbali ya nafasi za urais na makamu rais, Abdallah Mussa – aliyekuwa akiwania nafasi ya kugombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji TFF kutoka Kanda Na. 1 (Mikoa ya Kagera na Geita) aliondolewa kwa sababu ya kutoambatanisha kivuli cha cheti ya elimu ya sekondari.
Hivyo wagombea wa nafasi za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa kufuata Kanda 13 ni kama ifuatavyo:

No comments:

Post a Comment