KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 23, 2017

WAHAMIAJI HARAMU 45 WAKAMATWA WILAYANI MKINGA.

IDARA ya Uhamiaji Mkoani Tanga imewakamata wahamiaji haramu 45 kutoka nchini Ethiopia katika Kijiji cha Horohoro wilayani Mkinga mkoani Tanga kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria wakiwa shambani kwa wananchi wanakula mahindi kabla ya kutiwa nguvuni.

Licha ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao lakini pia idara hiyo inamshikilia raia mmoja kutoka
nchini Kenya ambaye ndio alikuwa akiwaongoza wahamiaji haramu hapa.


Akizungumza na waandishi wa habari,Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Crispin Ngonyani alisema wahamiaji
haramu hao walikamatwa June 18 mwaka huu katika kijiji hicho baada kupata taarifa kutoka
kwa wasamaria wema  wa eneo hilo.


Alisema wahamiaji haramu hao walikamatwa wakiwa porini katika jiji hicho wakati wakisafiri kuelekea nchini Afrika Kusini ambapo waligunduliwa na wananchi baada ya kufika mashambani mwao wakawakuta wanakula mahindi ndio walipotoa taarifa kwa askari wa Polisi wa Horohoro na hivyo wakaenda kuwakamata.

No comments:

Post a Comment