KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

August 18, 2017

KAMATA KAMATA, ZAIDI YA MADEREVA 100 WAKAMATWA DAR

untitled
Kamatakamata ya madereva pamoja na kutozwa faini na wengine kupelekwa Mahabusu kwa kushindwa kutii Alama za barabarani katika mitaa na barabara za katikati ya jiji iliyoanza jana, imeendelea kuwaweka katika wakati mgumu madereva wanaoendesha magari kwa kutozingatia alama za barabarani.
Majira ya Asubuhi katika mitaa ya jamhuri,zanaki na Mkwepu , Askari wa kikosi cha Usalama barabarani waliendesha Operesheni ya kukamata magari katika barabara hizo ambazo zimewekwa alama ambazo madereva walikuwa hawazifuati ama kwa kutojua au kwa makusudi.
Afisa Operesheni wa Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani Mkaguzi wa Polisi Cosmas Msigwa akizungumza na chanel ten katika mtaa wa Mkwepu amesema , zaidi ya madereva 100 wamekamatwa katika zoezi hilo majira ya asubuhi kwa kukiuka alama za barabarani.
Hata hivyo baadhi ya madereva walikumbana na zoezi hilo wamelitaka jeshi hilo kutoa elimu kwanza kabla ya kuwatoza faini lakini pia kubainishwa vizuri alama hizo ambazo wamedai ziliwekwa muda mrefu bila kutumika.CHANZO CHANNEL 10

No comments:

Post a Comment