KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 22, 2017

ASKARI 53 WAUAWA MISRI


Idadi ya wanajeshi na polisi waliouawa katika mapambano na wapiganaji wa Kiislamu katika eneo la Bahariya magharibi mwa jangwa imefikia 53, maofisa usalama na matabibu wamesema.

Wizara ya mambo ya ndani imesema vikosi vya usalama vilikuwa vinawasaka wapiganaji wa Kiislamu lakini waliviziwa katika chemchem ya maji ya Bahariya umbali wa kilomita 200 kusini mashariki mwa Cairo na kushambuliwa. Pia, imesema wapiganaji wa Kiislamu 15 wameuawa katika makabiliano hayo.

Vyanzo vilivyo karibu na maofisa usalama vinasema msafara huo ulishambuliwa kwa roketi na wapiganaji hao pia walitumia vilipuzi. Duru za usalama zinasema kuwa wapiganaji walikuwa na uelewa zaidi wa eneo hilo na ofisa wa jeshi aliyetoa amri ya kuvamia alishindwa kuagiza wanajeshi kuimarisha kikosi chake.

Hakuna kikundi chochote kilichodai kuhusika ingawa kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa juu ya wapiganaji wa kikundi kinachofahamika kama Hasm, kilichowahi kushambulia majeshi ya usalamasiku za nyuma. Hata hivyo, Twitter ya kikundi hicho inayotumiwa mara kwa mara kutoa taarifa haijafanya kazi tangu Oktoba 2.

Tangu jeshi lilipomwondoa madarakani Rais Mohamed Morsi wa Muslim Brotherhood, makundi ya kigaidi yameongeza sana mashambulizi yao dhidi ya wanajeshi na polisi.

Brotherhood, waliowahi kuwa kundi kubwa la upinzani nchini wamekanusha kuhusu katika machafuko.

Mohamed Morsi alichaguliwa kuwa rais mwaka 2012, lakini jeshi lilimpindua mwaka mmoja baadaye baada ya kuibuka maandamano ya kupinga sheria ya Kiislamu zinaosababisha mgawanyiko.

No comments:

Post a Comment