KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 23, 2017

KATALONIA WAKAIDI AMRI YA UHISPANIA


Catalan Estelada Maandamano ya kuunga mkono uhuru yalifanyika Barcelona siku ya Jumamosi
Viongozi wa jimbo la Catalania linalotaka kujitenga kutoka kwa Uhispania wamesema hawatafuata amri ya serikali kuu ya Uhispania iwapo serikali hiyo itachukua hatua za kulidhibiti jimbo hilo.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Catalonia Raul Romeva ameambia BBC kwamba serikali hiyo kuu inachukua hatua dhidi ya nia ya raia wa Catalonia.
Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy ametangaza mpango wa kuivunja serikali ya jimbo hilo na kupunguza baadhi ya uhuru ambao umekuwa ukijivuniwa na bunge la jimbo hilo.
Vyama vinavyounga mkono uhuru wa Catalonia vitakutana baadaye leo kujadili hatua za kuchukua.
Bunge la Seneti la Uhispania linatarajiwa kuidhinisha mikakati ya serikali hiyo Ijumaa pamoja na pendekezo la kufanyika kwa uchaguzi mpya katika jimbo la Catalonia.
Tulifikaje hapa?
Serikali ya Catalonia, ikiongozwa na Rais Carles Puigdemont, imekataa kusitisha juhudi zake za kutaka kujitangazia uhuru kutoka kwa Uhispania baada ya kuandaa kura ya maoni iliyokuwa imeharamishwa na mahakama nchini humo mapema mwezi huu.
Jumamosi, Bw Rajoy alisema atatumia Kifungu 155 cha katiba - katika hatua isiyo ya kawaida - ambacho kinairuhusu serikali kuu kutekeleza udhibiti kamili wa moja kwa moja dhidi mojawapo kati ya majimbo yaliyo na mamlaka ya kujitawala katika nchi hiyo iwapo kutakuwa na mzozo.
Lakini viongozi wa Catalonia wamesema hawataukubali mpango huo.
 BBC

No comments:

Post a Comment