Jana
nilikuwa nasoma gazeti moja, katika ukurasa wa mbele wameandika
“Asilimia 67 ya Watanzania wanatumia ARVs,” nilipo liona nikajua
wamekosea bahati mbaya nikaamua kufungua ndani nione kama walirekebisha.
Nilipofungua
ndani, nilikuta kichwa cha habari kile kile, nikasema ngoja nisome,
labda watakuwa wamerekebisha humu ndani, lakini habari ikawa vile vle
kuwa watanzania 67% wanatumia dawa za kufubaza makali ya virusi vya
UKIMWI.
Hayo
yamesemwa leo na Rais Magufuli alipokuwa anatoa wito wake kwa waandishi
wa habari nchini kuwa wazalendo na kuandika habari za kujenga kwani
akiandika habari za kupotosha, wanaichafua Tanzania.
Rais
alisema hayo kwenye hafla ya kutoa vyeti kwa wajumbe wa kamati
mbalimbali zilizohusika katika mchakato mzima wa madini, na kufanikisha
kufikiwa kwa makubaliano ambayo yameweka mwanzo mzuri wa serikali kuanza
kunufaika na rasilimali zake.
Rais
alisema baada ya kusoma hiyo habari alishtuka, na kuamua kumpigia simu
Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ili apate
ufafanuzi, na ndipo waziri akasema taarifa hiyo si ya kweli.
Waziri
Mwalimu alisema kuwa, alichokisema wakati wa Tsh 860 milioni kwa ajili
ya kununua dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI ni kwamba, jumla ya
watanzania milioni 1.4 wameathirika na virusi vya UKIMWI na kwamba
miongoni mwao (walioathirika), ni asilimia 67% pekee wanaotumia ARVs na
kwamba lengo la serikali ni kufika asilimia 90% ifikapo mwaka 2020.
Taarifa
hiyo iliandikwa kwatika gazeti la kila siku la TanzaniaDaima ambalo
hutolewa na Kampuni ya Free Media inayomilikiwa na Mwenyekiti wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe.
Rais
Magufuli alisema kwamba, taarifa kama hiyo inapoandikwa, inamadhara
makubwa kwa nchi kwani hata wawekezaji hawawezi kuja kwenye nchi ambayo
inaelezwa asilimia 67 ya watu wake wameathirika na UKIMWI kwa sababu
anajua hata akija hatopata nguvu kazi ya kutosha kufanyakazi kwenye
kiwanda/kampuni yake.
Lakini
pia alisema, taarifa hiyo inaweza kutishia hata watalii waliopanga kuja
kutembelea vivutio mbalimbali vya kitalii vilivyopo nchini Tanzania.
Katika
hatua nyingine, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William
Lukuvi amelazimika kutolea ufafanuzi kauli yake aliyoitoa akiwa
Sumbawanga mkoani Rukwa kuwa wale wote waliojenga katika maeneo ambayo
wamevamia au wamewadhulumu watu wengine, serikali itabomoa nyumba zao.
Waziri
amelazimika kutolea ufafanuzi kauli hiyo kutokana na magazeti ya leo
Oktoba 23 kuripoti taarifa hiyo kwa namna ya kuogofya, huku baadhi ya
vichwa vya habari vikisomeka, Bomoa Bomoa kubwa yaja (Nipashe), Bomoa
Bomoa ya karne yaja (Mtanzania).
Akiongezea
kwenye taarifa hiyo ya bomoa bomoa, Rais alisema kuwa waandishi hao
wangeweza wakaandika Waliojenga bila vibali kukiona cha moto na watu
wakasoma badala ya kuandika vitu ambavyo vinapotosha na kuwatia hofu
wananchi.
No comments:
Post a Comment