Serikali
kupitia mamlaka zake imezifungia rangi za midomo zinazozalishwa na
Mwanadada aliyewahi kuwa Miss Tanzania na Muigizaji wa Filamu, Wema
Sepetu. Rangi hizo zinajulikana kwa jina la "Kiss".
Kwa
mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) pamoja na Shirika
la Viwango Nchini(TBS) wamebaini kuwa rangi hizo hazina ubora kwa
matumizi ya binadamu.
Kwa
upande wa Meneja wa Wema Sepetu, Happy Shame alipotakiwa kuzungumzia
suala hilo amefunguka na kusema kwamba taarifa za kufungiwa kwa bidhaa
hizo yeye kama Meneja hajazipata bali anachofahamu mzigo ulikuwa
haujaingia sokoni na kwamba muigizajin huyo alikuwa bado akifuatilia
vibali kutoka mamlaka husika.
Rangi hizo za mdomo za muigizaji Wema Sepetu zilizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 usiku wa birthday yake.
No comments:
Post a Comment