KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

November 21, 2017

WALIOKWAPUA FEDHA SAUDI ARABIA WATAKIWA KUREJESHA

Mamlaka za Saudi Arabia zimewataka watoto wa kiume wa familia za kifalme na baadhi ya wafanyabiashara wanaoshikiliwa kurudisha mali walizojipatia kwa njia isiyo halali ili waweze kuachiwa huru, vyombo vya habari vimeripoti.

Shirika la habari la Bloomberg limesema watu 201 wakiwemo wafanyabiashara, mawaziri na wana wa ufalme miongoni mwao mwana mfalme Alwaleed bin Talal anayemiliki jengo refu la ghorofa katika mji mkuu, Riyadh wanashikiliwa na mamlaka za Saudi Arabia katika kampeni yake ya kukabiliana na rushwa. Pia, mamlaka zimefunga akaunti zao za benki.

Taarifa za vyombo vya habari zinasema kuwa mamlaka nchini Saudi Arabia zimewataka wanaoshikiliwa kurudisha mali walizopata kwa njia ya rushwa ikiwa wanataka kuachiwa huru na wasifunguliwe mashitaka. Inakadiria kuwa kati ya dola za Marekani 50 bilioni na 100 bilioni zitahamishwa kwenda hazina ya taifa.

Mapambano dhidi ya mafisadi yanaongozwa na mwana mfalme Mohammed bin Salman anayejaribu kuimarisha nguvu yake ya kimamlaka kabla ya kuapishwa rasmi kuwa mrithi wa ufalme.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaamini kuwa anataka kukusanya fedha anazohitaji kwa ajili ya kufanya mageuzi ya kiuchumi nchini.

No comments:

Post a Comment