KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

December 12, 2017

WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU ATEMBELEA ZAHANATI YA MHANDU WILAYANI MSALALA

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto aweka historia kwa kutembelea Zahanati ya Mhandu kata  ya Chela Wilayani Msalala ambapo tangu Uhuru wa Tanzania kijiji hicho hakijawahi kutembekewa na Kiongozi wa Kitaifa.
Waziri Ummy Mwalimu yupo ziara ya kikazi Wilayani Msalala kujionea Utekelezaji wa  Mpango wa Malipo kwa Ufanisi(RBF) ambapo ulianza Januari 2016 kwa Mkoa wa  Shinyanga
RBFni Mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi ambapo vituo vinapewa maeneo ya utekelezaji na kupimwa kuona kama wamekidhi na kufikiwa malengo hivyo kituo huhakikiwa na hatimaye kutolewa fedha kulingana na matokeo ya idadi za huduma zilizotolewa na ubora kulingana na miongozo ya utoaji wa huduma za Afya.
Fedha zinazopatikana zinafanya maboresho ya vituo ikiwemo miundombinu ya kituo,madawa na vifaa tiba
Waziri Ummy Mwalimu ameipongeza halmashauri ya wilaya hiyo kwa kufanya vizuri katika kutekeleza Mpango huo hata hivyo aliwataka watendaji kufanya uhakiki na kujiridhisha kwamba huduma za Afya zitolewazo zinakidhi viwango kulingana na miongozo ya Afya ndipo malipo yatolewe
Alisema Mpango huo unahakikisha huduma ya Afya ya msingi zinatolewa bila vikwazo,”nimekuja kufuatilia utekelezaji kwakweli nimefurahi kwani mnatekeleza na mmeboresha huduma zenu”
Aidha,alisema kabla ya utekelezaji wa Mpango huo kuanza mwaka 2015 hali ya miundombinu ilikua mibovu,hakukuwa na dawa,hivyo kupitia Mpango huo Serikali hupeleka fedha ambazo zinasaidia kuimarisha mifumo ya vituo vya Afya,kuongeza huduma za huduma,kuchochea jamii kutumia vituo vya Afya hususan wanawake wajawazito pamoja na kutoa motisha kwa wahudumu na watumishi wa Afya katika vituo vya kutolea huduma.
“Mpango huu tunataka wanawake wajawazito waje vituoni ndani ya miezi mitatu ya mwanzo na serikali tunaleta shilingi 8290,na mjamzito akihudhuria kliniki angalau Mara NNE wakati wa ujauzito tunaleta shilingi 6210 kwenye zahanati” alisema Waziri Ummy
Alitaja kiasi cha shilingi 20,700 serikali inatoa kwa mjamzito akienda kujifungua kwenye Zahanati hivyo alitoa ari kwa wanawake wajawazito wilayani Msalala kuacha kwenda kujifungua kwa wakunga wa jadi kwani Serikali ya awamu ya tano imeboresha huduma za Afya nchini ikiwemo hali ya  upatikanaji wa dawa ambapo Msalala kwa mwaka wa fedha 2017/2018 wametengewa shilingi milioni 417 tofauti na ile ya mwaka 2015/2016 ya shilingi milioni 108.

No comments:

Post a Comment