Mpiga picha wa msanii Diamond Platnumz na WCB kwa ujumla, Kifesi ameamua kuachana na kazi hiyo.
Kifesi
ameeleza kuwa muda aliyofanya kazi WCB wa takribani miaka mitano
unatosha ila kilichomsukuma zaidi kuacha kazi ni kutaka kujiajiri na
kuwa karibu na Mungu wake kwani kazi aliyokuwa anaifanya ilimbana zaidi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kifesi ameandika;
"Leo
ikiwa ni siku takatifu na siku ya ibada kwangu ni siku nilioamua
kufanya maamzi yatayobadili maisha yangu, nimeamua rasmi kuacha kazi
kama mpiga picha wa Diamond na mwajiriwa wa WCB..
"Well
It’s insane to be leaving a stable job u love But that’s reality for me
naacha kazi kwa mtu alikuwa zaidi ya Rafiki kwangu, naacha kazi ambayo
ni ndoto ya vijana wengi out there but to me..i see miaka yngu 4/5 ya
kufanya kazi hapa inatosha niachie nafasi kwa vijana wengine nimeamua
kufata moyo wangu.
"Ni
uamzi niliokua nao karibu mwaka sasa but kama ilivyo kwa waajiriwa
wengi is so hard kufanya maamzi ya kuacha kazi but IN ORDER TO GROW WE
NEED TO MAKE CHANGE.. Naacha kazi to pursue my Dreams life ikiwamo
kujiajiri mwenyewe. Naacha kazi ili nipate muda mwingi wa kuwa flexible
nitumie muda wangu mwingi ku-unleash my potential for excellence.
reason ya mwisho na kubwa zaid kwangu.
"Naacha
hii kazi ili niwe karibu zaidi na Mungu wangu kwa imani yangu kama
Mkristo nilikua nafanya kazi katika lifestyle na mazingira ya kazi
yasiyompendeza Mungu, ilinibidi kujihusisha na mziki, kwenda kwenye
matamsha ya mziki, kwenda maeneo ya starehe kutokua na muda wa kwenda
kanisani sababu ya kazi at the end we need to choose GOD over
everything, sifa, umaarufu na fahari yote ya Dunia vitanifaidia nini
endapo nitaukosa ufalme wa Mungu.
"Nimeamaua
ku-drop kila kitu i just want to be happy, do my works live my life and
have time with God, ukimchagua Mungu hata hivi vingine atakuongezea
najua kutakua na changamoto nyingi, Up and downs but Mungu He knew me
before was born aliahidi ukimchagua yeye he will open the doors
atatufnya kuwa kichwa na siyo mkia.
"Mwisho
nashukuru familia yote ya WCB kwa kuwa na mimi for all these years was
great working with u.. but zaidi nimshukuru Diamond kwa muda wote
niliofanya nae kazi since chini mpaka sasa, nimefnya kazi kwa mapenzi,
bidii na uaminifu mkubwa kwangu haukua boss bali rafik na nilkua rafiki
wa kweli kwako a will always appreciate mchango wako kwangu..
Tusameheane pale tulipowahi kukoseana we are just humans, hatutakuwa
pamoja kikazi but nina imani tutaendelea kuwa marafiki. God bless you,
uzidi kufika unapopenda kufika, GOD Bless me.. God bless my next Hustles
#happysabbathDay
Utakumbuka
Siku chache zilizopita, March 28, 2018 mara baada ya aliyekuwa Baby
Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady kupata dili la kuwa balozi
wa bidhaa za Softcare Diapers, Kifesi alitupa lawama kwa Diamond kwa
kumuacha Zari kwa kudai alikuwa ni mwanamke wa Baraka aliyepewa na
Mungu.



No comments:
Post a Comment