WAFANYAKAZI
watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) jana walifikishwa
mahakamani kwa kosa la kuisababishia hasara serikali ya dola za
Kimarekani 35,500 (sawa na Sh. milioni 79).
Watuhumiwa
waliofikishwa kizimbani na kusomewa mashtaka ni Joseph Mtwala (36),
John Mlambo (42), Mwahu Yunus (38), Mery Njau (38) na Catherine Edward
(33).
Watuhumiwa
kwa pamoja walisomewa shtaka moja na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru), Adamu Kilongozi akisaidiwa na
Hamidu Simbano na Richard Jacopiyo alidai kuwa walitenda kosa hilo kati
ya Desemba 25, mwaka 2013 na Juni 6, mwaka 2014.
Kilongozi
alidai kuwa watuhumiwa hao wakiwa katika lango la Nabi mkoani Mara na
lango kuu la Loduare mkoani Arusha walisababishia serikali kiasi hicho
cha hasara wakiwa watumishi wa NCAA.
Mwendesha
mashtaka huyo alisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya
Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Bernard Nganga, na kudai kuwa walifanya
kosa hilo wakijua ni kinyume cha sheria.
Kilongozi aliiambia mahakama kuwa ushahidi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba ipangiwe tarehe ya kuanza usikilizwaji wa awali.
Watuhumiwa
wote walikana shtaka hilo na walipewa masharti ya dhamana ya kila mmoja
kuwa na wadhamini wawili kila mmoja Sh. milioni 7.9 au mali
isiyohamishika yenye thamani hiyo.
Hata hivyo, wadhamini hawakukamilisha masharti hayo jana, hivyo washtakiwa kupelekwa mahabusu hadi Aprili 10, mwaka huu.



No comments:
Post a Comment