KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

March 20, 2018

WAFUNGWA KUPEWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI HUKO GEREZANI ILI KUWASAIDIA KUBAINI FURSA MBALIMBALI ZA KIUCHUMI

Na Lucas Mboje, Jeshi la Magereza;
Jeshi la Magereza limetiliana saini makubaliano na Asasi ya TECHNOSERVE katika kuendesha  mafunzo ya ujasiriamali kwa wafungwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 30 waliopo magerezani katika Mikoa ya nyanda za juu Kusini ikiwemo Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma, Katavi na Rukwa.

Hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo imefanyika katika Ofisi za Makako Makuu ya Jeshi la Magereza jijini Dar es Salaam na Asasi ya TECHNOSERVE iliwakilishwa na Afisa wake Bw. Monsiapile Kajimbwa.

Akizungumza baada ya kutiliana saini makubaliano hayo, Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa amesema kuwa mafunzo hayo ya ujasiriamali yatawapa uwezo wafungwa wa kubaini na kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo uwezo wa kubuni na kuandaa mipango ya biashara.

“Mafunzo haya yatawanufaisha sana wafungwa waliopo magerezani katika mikoa hiyo kwani yatawajengea uwezo wa kujitambua pamoja na kujipatia vipato halali badala ya kutenda uhalifu katika jamii.” Alisema Jenerali Malewa.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo yatafanyika katika Chuo cha Ufundi cha Magereza Ruanda kilichopo Mkoa wa Mbeya ambapo wafungwa watajifunza nadharia na vitendo katika dhana nzima ya ujasiriamali ikiwemo stadi za utengenezaji sabuni, ushonaji, useremala, ufumaji sambamba na uandaaji wa mipango ya kibiashara.

Meneja Mkazi wa Asasi ya TECHNOSERVE, Bw. Monsiapile Kajimbwa amesema kuwa hatua ya kutiliana saini makubalino hayo ni kuimarisha ushirikiano kati ya Asasi yake na Jeshi la Magereza katika kutoa mafunzo kwa wafungwa ili waweze kupata ujuzi kupitia program hiyo.

Dira ya Jeshi la Magereza ni kuwa Jeshi la kurekebisha wahalifu lenye utaalam wa hali ya juu linaloendeshwa katika kanuni na viwango vilivyowekwa Kitaifa na Kimataifa.

No comments:

Post a Comment