Wasanii
wa bongo fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’na Faustina Charles
‘Nandy’ wamewasili katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).
Wasanii hao wanaitikia wito wa TCRA ikiwa ni siku chache baada ya kusambaa kwa video zao zinazokiuka maadili.
Nandy
aliwasili TCRA saa 5:48 asubuhi leo Aprili 19 na Diamond aliwasili saa
6:15 mchana. Diamond alisindikizwa na menejimenti yake ikiongozwa na
Said Fella.
Hivi
karibuni, Waziri wa Habari, Sanaa na Utamaduni, Dk Harrison Mwakyembe
alizungumza bungeni kuwa wasanii hao walikamatwa na kuhojiwa kuhusu
kusambaa kwa video zinazokiuka maadili.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alithibitisha kuwahoji wasanii hao.



No comments:
Post a Comment