Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro amefunguka na kudai
anashukuru kuona baadhi ya wahalifu nchini wameanza kuelewa juu ya kauli
yake ya 'uhalifu haulipi' huku akiendelea kuwasisitizia wengine ambao
bado wanaendelea kujishughulishia na mambo hayo kuwa wasije kuilaumu
serikali
IGP
Sirro ametoa kauli wakati alipokuwa amefanya ziara ya kushtukiza kwenye
kambi ya Jeshi la Polisi mkoani Morogoro kwa lengo la kutaka kujua
changamoto na hali walizokuwa nazo askari ndani ya kambi hiyo ili mradi
aweze kushughulikia mapungufu atakayokumbana nayo.
“Mtu
yeyote au kikundi chochote kisitishie amani ya nchi kwa manufaa yake,
watu watii sheria na atakayekwenda kinyume cha sheria sheria
itamshugulikia.
"Watu
wengi wanapenda kutii sheria ila ni wachache sana wanapenda kuingia
kwenye uhalifu na mtu akiingia kwenye uhalifu lazima nitamshugulikia.
"Kuna
watu wengine wanataka waone wapi kuna upungufu ambapo askari hawafanyi
kazi vizuri ili waweze kufanya uhalifu wao, na huwa ninasema siku zote
uhalifu haulipi. Utapiga bunduki, utaiba leo, kesho ukiingia mahali
pabaya usilaumu serikali", amesema IGP Sirro.
Aidha,
IGP Sirro amesema sasa hivi kila mhalifu akitaka kuchukua bunduki
kuenda kufanya tukio huwa anajiuliza mara mbili mbili kama ataweza
kurudi salama huko aendapo.
Kwa
upande mwingine, IGP Sirro amesema hapendi kumuona askari polisi akiwa
legelege kwa kuwa akiwa hivyo atoweza kumlinda raia ipasavyo.



No comments:
Post a Comment