KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 27, 2018

LADY JAYDEE AFIWA NA MAMA YAKE

Mama mzazi wa msanii wa muziki wa bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee, Bi. Martha Mbibo, amefariki dunia alfajiri ya leo.

Akithibitisha taarifa hizo kaka wa Lady Jaydee ambaye pia ni msanii Dabo, amesema kwamba mama yao amefariki akiwa nyumbani kwake baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.

Dabo amesema msiba upo nyumbani kwa marehemu Jet jijini Dar es salaam, na familia itatoa utaratibu wa mazishi mara baada ya utaratibu wa kuupeleka mwili hospitali kuhifadhiwa kukamilika.

No comments:

Post a Comment