Mbunge
wa Viti Maluum (Chadema), Lucy Magereli amesema uamuzi wa Rais John
Magufuli kununua ndege hauwezi kuwa sababu ya kulifufua Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL).
Akizungumza
katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
mwaka 2018/19, mbunge huyo amesema kuliko kununua ndege hizo, Serikali
ingekodisha ndege na kuanza kujipanga taratibu kuliboresha shirika hilo.
“Nani
aliyemshauri Rais kununua ndege? Tungeweza kuifufua ATCL kwa ndege za
kukodi, hatuhitaji ndege kubwa. Hivi tunawezaje kushindana na mashirika
makubwa ya ndege duniani ambayo yapo muda mrefu na yamejiimarisha,”
amesema.
“Suala
si kuhitaji ndege, suala tumezipata kwa utaratibu upi. Tuna ndege
wakati viwanja vya ndege vya ndani havifai kwa matumizi yetu. Leo mtalii
akitua Dar es Salaam akitaka kwenda maeneo mengine atafika kwa shida.”
Mbunge
huyo alihoji sababu za Serikali kununua ndege kubwa wakati
haijaimarisha miundombinu, vikiwemo viwanja vya ndege, “ndege
tunazonunua ni mzigo kwa nchi hii, zinahitaji matengenezo, tutayaweza?”
“Kesho
na keshokutwa Bunge litakaa tena na kusema tumetumia fedha nyingi
kuifufua ATCL na kuliingiza Taifa katika matatizo. Nawaambieni tutakaa
hapa kujadili tena jambo hili.”
“Tumetumia fedha nyingi kukomboa ndege zetu zilizozuiwa Canada je hizo fedha Bunge gani limezipitisha?” Amehoji.



No comments:
Post a Comment