Basi
la kampuni ya Saratoga lililokuwa likitoka mkoani Kigoma kwenda
Sumbawanga limeshika moto na kuteketea lote katika eneo la kijiji cha
Kazuramimba mkoani Kigoma leo asubuhi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP Martin Ottieno amesema kuwa jeshi lake bado linachunguza chanzo cha moto huo, ambapo amebainisha kuwa abiria wote sitini wamepona na baadhi ya mizigo imeokolewa.
“Gari
limekaguliwa kabla ya kuondoka katika stendi ya mabasi kama kawaida ya
utaratibu wa kikosi cha usalama barabarani na hakuna tatizo
lililoonekana, hivyo chanzo cha moto huo bado hakijajulikana tunafanya
uchunguzi”, amesema Kamanda Ottieno.
Basi
hilo limeungua ikiwa ni siku moja toka mtu mmoja kupoteza maisha katika
ajali ya moto ulioteketeza malori katika mpaka wa Tanzania na Rwanda
(Rusumo), baada ya gari la mafuta ya petrol kuligonga gari jingine na
kupoteza mfumo wa breki.
No comments:
Post a Comment