KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Dk.Bashiru Ally amesema CCM
inaendelea kuimarika na hakuna Chama chochote cha kisiasa nchini
kinachoweza kushindana nacho katika uringo wa siasa za ushindani wa sera
za maendeleo kwa wananchi wa makundi yote.
Kauli
hiyo aliitoa mara baada ya kuwasili kisiwani Pemba katika mwendelezo wa
ziara yake ya kujitambulisha ambapo amezungumza na wanachama mbalimbali
katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Fidel Castro Wilaya ya Chake
Chake Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema
kutokana na uimara huo hakuna chama kingine mbadala wa Chama Cha
Mapinduzi kinachoweza kushuka kwa wananchi nyumba kwa nyumba na kuratibu
kero zao kisha kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Dk.Bashiru
aliwahakikishia wanachama na viuongozi hao kuwa CCM bado ipo imara na
itapata ushindi wa kihistoria mwaka 2020 kwa nchini nzima kuliko ushindi
unaopatikana kwa sasa katika uchaguzi mdogo unaoendelea katika maeneo
mbalimbali nchini.
Aliongeza
kwamba sababu za kushinda na kusambaratisha upinzani zipo kwani vyama
vya upinzani nchini vimekosa muelekeo na ndio maana wanachama wake
wanahamia CCM kwa wingi.
Alisema
Tanzania inahitaji vyama vya siasa imara vitakavyolinda na kuhubiri
misingi ya utaifa na umoja na msikamano wa Tanzania, bila ya kujali
tofauti za kisiasa.
Kupitia
mkutano huo aliwambia wanachama wa vyama vya upinzania kisiwani Pemba
kwamba huu ndio wakati wao wa kujitawala kifikra kwa kujiunga na CCM
kwani Chama Cha CUF hakina tena mvuto kwa jamii kutokana na tabia ya
unafiki na uongo inayofanywa na viongozi wakuu wa Chama cha CUF.
“Wanachama
wa vyama vya upinzani njoo CCM huku tupo shwari na tumekamilika kila
idara wala msihofu chochote hakuna mtu yeyote wa kuwagusa, na wale wote
waliojiunga na chama chetu leo nahakikishieni kuwa mtafaidika na siasa
safi na demokrasia iliyotukuka.
Pia
Wana-CCM wenzangu awa wenzetu wanaojiunga na CCM wapokeeni na
kuwathamini kwani wamefanya maamuzi sahihi ambayo hawatoweza
kuyajutia.”, alisema Dk.Bashiru.
Dk.Bashiru
kupitia mkutano huo alitangaza rasmi kuwa Chama Cha Mapinduzi
kitaendelea kuvunja ngome zote za upinzani kabla ya mwaka 2020, kutokana
na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM ya mwaka
2015/2020.
Alisema
dhamira ya tasisi hiyo kwa sasa ni kuendeleza kwa vitendo mambo mema
yaliyoasisiwa na vyama vya ukombozi vya ASP na TANU vilivyoungana na
kuzaliwa kwa CCM.
Pamoja
na hayo aliweka wazi kuwa kila kila mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi
anatakiwa kulinda Muungano, Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kwani
tunu hizo ndio chimbuko la mafanikio yaliyopo hivi sasa.
Kupitia mkutano huo pia Dk.Bashiru aliwapokea wanachama wapya 62 waliotoka chama cha CUF na kujiunga na CCM kisiwani Pemba.
Aliwapongeza
wanachama wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kumuamini
kasha kupendekeza ateuliwe kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM
Tanzania, na akaahidi kuwa atatumia nafasi yake kuleta mageuzi makubwa
ya kimaendeleo ndani nan je ya CCM.
Akizungumza
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla (Mabodi),
alisema kazi kubwa ya Chama cha mapinduzi kwa zama za sasa ni kutekeleza
kwa vitendo dhana ya CCM mpya na Tanzania mpya kwa maendeleo ya jamii.
Alisema
miradi mbali mbali ya maendeleo iliyotekelezwa kwa ufanisi kisiwani
Pemba ikiwemo mfuko wa maendeleo wa TASAF na kuongeza bei ya zao la
karafuu ni kutokana na utekelezaji mzuri wa sera za CCM.
Naye
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Ndugu Yussuf Ali Juma alisema
ndani ya Mkoa huo wanaendelea na mikakati ya kuhakikisha CCM inashinda
kwa ngazi zote katika uchaguzi Mkuu ujao.
Katika
ziara hiyo Dk. Bashiru alifuatana na viongozi mbali wa Chama na Jumuiya
wakiwemo wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, wajumbe wa halmashauri Kuu
ya CCM Taifa, Makamu Wenyeviti wa Jumuiya pamoja na viongozi mbali
mbali wa Chama na Serikali Zanzibar.
No comments:
Post a Comment