Mchekeshaji
Idris Sultan amempongeza Mwanamitindo Hamisa Mobetto kuingia kwenye
muziki. Idris amesema yeye anamsapoti Hamisa na anashangazwa na wale
wanaomkeli kwa hatua hiyo.
==>>Kupitia ukurasa wake wa Instagram Idris ameandika;
"Naomba
niwe kati ya wale wa kwanza kukusapoti ili ukija kuanza kuchukua matuzo
usitusahau maskini wenzio. Mwanzo sio mwepesi ila kama msimamizi wa
mpesa vodacom naweza sema yajayo yanafurahisha. Nitashangaa kuona watu
wanakukejeli kwenye hii hatua yako katika upiganaji sijui wanataka
ukatembee barabarani unauza nanilii sasa.
"Katika
hatua za mafanikio jua sana kuchuja maneno. Kama kweli umedhamiria
kufanya mziki basi kazaaa na unatoboa tu kwani hao wengine ni kina nani
labda. Wengine tulianza hatukubaliki hata tutoe msaada wanguo zetu
tutembee watupu ila unakaza tu na baada ya mda unaanza okota fan mmoja
mmoja wawili mwishowe una mamilioni #RefuseToStop"
Jana August 20, 2018 Hamisa Mobetto ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jila na Madam Hero.
Hamisa
ni mrembo mwingine Bongo kujaribu bahati yake kwenye Bongo Fleva baada
ya wengine kama Wema Sepetu, Jokate Mwegelo Aunt Ezekiel nakadhalika.
No comments:
Post a Comment