Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro ametoa onyo kali kwa
majambazi na wahalifu wengine hususani wanaotumia silaha za moto kuacha
mara moja kabla ya kukutana na moto mkali wa Jeshi la Polisi ambapo pia
ametoa wito kwa wazazi kuwakanya watoto wao kujihusisha na vitendo
hivyo.
IGP Sirro ameyasema hayo wakati akizungumza na Wakazi wa Mto wa Mbu Tarafa ya Manyara Wilayani Monduli Mkoani Arusha wakati wa Ziara yake mkoani humo yenye lengo la kubaini changamoto za kiuhalifu na kuzitafutia ufumbuzi.
Alisema
hivi sasa ujambazi wa kutumia silaha umepungua kwa kiasi kikubwa na
baadhi ya matukio ambayo yamekuwa yakijitokeza yanaendelea kudhibitiwa
na Jeshi la Polisi.
“Nawasihi
wanaofikiria kuendelea kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo vya utumiaji
wa silaha na kuua watu waache mara moja kwa kuwa wakikutana na moto wa
Jeshi la Polisi wasije wakajilaumu mana kwa sasa moto wetu ni mkali
hivyo nawashauri wazazi wakanye watoto wao” Alisema Sirro.
Aidha
amewataka Wakazi wa Mto wa mbu Wilayani Monduli kuendelea na shughuli
zao kama kawaida kwa kuwa usalama umeimarishwa katika kupambana na
wahalifu waliokuwa wakifanya vitendo vya kuwaua watu hususani wanawake
ambapo katika kipindi cha hivi karibuni kuliripotiwa matukio kadhaa
ambayo yalileta wasiwasi katika eneo hilo muhimu kwa utalii.
Amewataka
Viongozi wa Vijiji na Kata kuhakikisha kuwa suala zima la ulinzi na
usalama linatiliwa mkazo ili kuhakikisha hakuna mhalifu katika maeneo
yao na wageni wanapoingia wachukue taarifa zao mapema.
Kwa
Upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Mto wa Mbu Bi. Kuluthum Hassan
alisema Wahalifu wanaouza bangi, pombe ya gongo na dawa za kulevya
wanaendelea kuwafichua ili wafikishwe katika vyombo vya dola na hivi
sasa wanaendelea na mipango ya ujenzi wa kituo kikubwa cha Polisi
kitakachoendana na hadhi ya eneo hilo.
No comments:
Post a Comment