Mkazi
wa kijiji cha Kinku tarafa ya Mungaa wilaya Ikungi , Singida, Editha
Kanisi (49) ameuawa kwa kukatwa kwa kisu cha kukatia majani, (mundu)
shingoni na kichwani na mume wake Joseph Wilbroad (53).
Baada ya Joseph kufanya mauaji hayo wananchi wenye hasira kali nao walimshambulia kwa silaha na kumuua.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jana Agosti 16 Kamanda wa Jeshi
la Polisi mkoa wa Singida, ACP Sweetbert Njewike alisema tukio hilo
limefanyika Agosti 15 mwaka huu usiku saa mbili huko katika kijiji cha
Kinku.
Alisema
kuwa tukio hilo lilitokea usiku wakati wanandoa hao wakijiandaa
kulala na uliibuka mzozo mkali baina yao huku kila mmoja akimtuhumu
mwenzake kuwa si mwaminifu kwenye ndoa.
“Kila mmoja alimtuhumu mwenzake kutokuwa mwaminifu katika ndoa yao,”alisema.
Akifafanua
zaidi alisema malumbano hayo yalisababisha mwanaume kuchukua kisu cha
kukatia majani kiitwacho mundu na kumkata mke wake shingoni na kichwani.
Alisema Editha alijaribu kukimbia lakini alipotoka nje ya nyumba yao alianguka chini na kufariki dunia papo hapo.
“Watoto
wao baada ya kuona mama yao kaanguka chini, walianza kupiga kelele za
kuomba msaada na majirani walifika mara moja kwenye eneo la tukio na
wakamwomba Joseph afungue mlango,” alisema Kamanda huyo
"Joseph
alikaidi kufungua mlango na ndipo walipouvunja kwa nguvu.Walipofanikiwa
kumkamata Joseph,walimpiga kwa silaha za jadi na kusababisha kifo
chake,”aliongeza.
Alisema uchunguzi zaidi na msako mkali unaendelea kuwasaka waliohusika na mauaji ya Joseph.
No comments:
Post a Comment