"Narudi kwetu kwa ajili ya kuwatumikia wanananchi,narudi Muleba jimboni kwangu kuwahudumia wananchi, sina maneno mengi ila namshukuru Rais kwa kunipa nafasi ya kulitumikia taifa," anasema Prof.Anna Tibaijuka baada ya kuwasili mjini Bukoba. Akasema alipokea fedha hizo bila kujua kama zimetoka kwenye akaunti ya Escrow ndiyo maana alizipokea.Rais Jakaya Kikwete akiongea na Wazee wa Jiji la Dar es Salaam alisema amemuomba Prof.Tibaijuka ambaye alikuwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi apumzike ile atoe nafasi kwake (Rais) kumteua mtu mwingine.
No comments:
Post a Comment