KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

December 24, 2014

BAADHI YA WANANCHI KAGERA WAPINGA PROF.TIBAIJUKA KUTIMULIWA PEKE YAKE, WAHOJI KWANINI WENGINE WAWEKWE KIPORO, NAYE AZUNGUMZA BAADA YA KUTOSWA

Baadhi ya wananchi mkoa Kagera wamepinga uamuzi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumuondoa madarakani Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi na kuwaweka kiporo viongozi wengine walioshiri kuhujumu pesa za akaunti ya Tegeta Escrow.
Prof.Tibaijuka
Nao baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya mkoa huo akiwemo Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kagera, Hamim Mahamoud amepongeza uamuzi wa Rais alioutoa jana kwa kumuondoa kiongozi huyo.
Kwa upande wake, Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Manispaa ya Bukoba, Victor Sherejei akisema kuwa Rais hajatoa uamuzi sahihi. Amemtaka Rais kuwafahamisha Watanzania ni lini pesa za Escrow zitarudishwa katika akaunti hiyo. Akahoji ikiwa kuwaondoa viongozi hao madarakani ndiyo suluhisho la kwamba pesa hizo hazirudishi?

Naye Profesa Anna Tibaijuka amesema baada ya Rais kumuondoa katika nafasi yake aliyokuwa nayo, sasa amerudi jimboni kwake kwa ajili ya kutatua kero na changamoto mbalimbali za wananchi wake kwani nafasi aliyokuwanayo ilikuwa haimpi nafisi ya kuwasimamia wananchi katika jimbo lake na kwamba, pesa hizo alizopewa na Rugemarila zilikuwa za kusaidia shule na alipewa kama zawadi bila kujua kama pesa hizo zilitoka katika akaunti ya Tegeta Escrow, ndiyo maana hakutaka kujiuzulu.

No comments:

Post a Comment