MWIGIZAJI na mwanamuziki wa Bendi ya FM
Academia, Patcho Mwamba hivi punde ameibuka katika ofisi za mtandao huu
na kukanusha vikali taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa
amefumaniwa akiwa na mke wa mtu na kupokea kipigo.
Akiongea na mtandao huu, Patcho amesema picha iiliyozagaa mitandaoni
aliipost mwenyewe juzi baada ya kupata aleji ya macho ambapo baadaye
ilisambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa kapigwa baada ya fumanizi.
"Unajua nina aleji na pombe pamoja na vumbi, nikitumia tu pombe lazima macho yangu yavimbe
juzi nilikunywa Windhoek mbili na usiku hali yangu ikabadilika na macho kuvimba, baada ya tukio hilo niliamua kujipiga picha na kuipost katika mtandao wa Instagram na hapo ndipo balaa likazuka" Alisema Patcho akiwa katika ofisi za mtandao huu zilizopo Mwenge-Bamaga, Dar.

MZUSHI KWENYE MTANDAO ALIANDIKA HIVI:Wakati wengine wakisheherekea sikukuu ya Christmass duniani kote ikiwa ni kumbukumbu kwa wakristo wote kuzaliwa kwa Mwokozi wao "YESU" Wengine siku hiyo wanaifanya kuwa siku ya starehe na kufanya mambo kinyume na maana ya siku yenyewe. Msanii wa filamu za bongo maarufu kwa jina la Pancho Mwamba, anadaiwa kufanyiwa mbaya baada ya fumanizi siku ya Xmass. Msanii huyo inasemekana amefumaniwa na mke ambaye si wake siku ya Christmass maeneo ya Kinondoni jijini hapa.
No comments:
Post a Comment