Mh.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik na kulia ni katibu wa Baraza la wazee wa Dar es Salaam Mzee Mtulia. |
Serikali iliahidi Mkaguzi na Mdhidhiti wa serikali (CAG) kufanya ukaguzi na PCCB kuchunguza na kuchukua hatua stahili.
Alisema CAG alifanya ukaguzi na taarifa kuwasilishwa Bungeni, na aliagiza taarifa hiyo ichapishwe kwenye magazeti na tovuti ya serikali.
"Takukuru wameendelea na uchunguzi wao,na matokeo yake huwa ni watu kufikishwa mahakamani" alisema Mkurugenzi wa PCCB alitoa ushirikiano wake.
Rais alisema kutokana na hali yake ya ugonjwa ufuatiliaji wa suala hilo ulichukua muda sababu ilibidi kwanza apumzike baada ya kutoka Marekani kwa matibabu.
Alisema katika kununua umeme Tanesco inaingia mikataba, mikataba iko ya aina mbili, wa kwanza ni mkataba wa tozo ya umeme (energy charge) haya ni malipo ya umeme walioununua kutoka kampuni husika,malipo ya pili ni Tozo ya uwekezaji (capacity charge) haya ni malipo ya kulipia gharama za uwekezaji . Alisema katika makubaliano hayo wanaweka utaratibu wa kushughulikia matatizo au mizozo yao, wakishindwa wanatafufa mshauri,lakini hayo mawili yakishindikana wanakwenda kwenye kituo cha kimataifa cha usuluhishi London Uingereza.Na uamuzi wake ni wa mwisho na hauna rufaa.
Alifafanua kuwa mwaka 1998 walifikishana kwenye kituo hicho kama mahakama, Tanesco ikilalamikia tozo ya uwekezaji IPTL inawalalia, wanatoza tozo kubwa kuliko uwekezaji uliopo, Mahakama hiyo ilikubaliana na Tanesco na uamuzi ukawa kupunguza tozo ya uwekezaji ambayo ambayo IPTL ilikuwa inaitoza Tanesco kutoka dola milioni tatu na ushee hadi mbili na ushee.
Kutokana na mzozo huo kutatuliwa Tanesco hawakuridhika bado, wakaamua kukubaliana kufungua akaunti ya Escrow pale Benki kuu, walifanya makubaliono hayo.. masharti ya akaunti ile yakawa ni kwamba IPTL itaendelea kupeleka madai yake Tanesco ya Tozo ya Uwekezaji na kuendelea kulipwa lakini tofauti na zamani malipo hayo yatakwenda kwenye akaunti ya Escrow wakisubiri Tanesco na IPTL wamalize tofauti zao, lakini fedha zile nyingine za uzalishaji umeme IPTL ilikuwa inalipwa.
Alisema kwa miaka saba Tanesco ilikuwa inapeleka fedha Escrow... sasa kwa mujibu wa CAG tarehe 20 Novemba akaunti ilikuwa na Shilingi bilioni 8.2 Hati Fungungani zilikuwa na thamani ya Bilioni 181 na ushee na dola za marekani 22 milioni jumla ni bilioni 202.9 .....
Kwa mijibu wa mkataba, Tanesco wasipolipa kwa wakati kuna riba ya asilimia mbili, na kwamba Tanesco ilikuwa inadaiwa dola milioni 33.6 na ushee.
Wakati akaunti inafungwa kwa amri ya mahakama ilikuwa na Sh.Bil. 202.kati ya bilioni 306 .7 ambazo Tanesco walipaswa kulipa,zilizosalia ni deni.
"Maelezo haya yanasaidia kupata jibu la swali maarufu kwamba hizi fedha ni za nani, ni za umma au za ITPL,"
Akifafanua zaidi ya juu ya akaunti ya Escrow, alisema ni akaunti maalum inayoanzishwa kwasababu maalum kufanya kazi maalum kwa masharti maalum na kwamba tatizo likiisha akaunti inafungwa na husimamiwa na wakala kwa makubalino ya wanaofungua akaunti hiyo, na wakala ndiye mwenye jukumu la kuisimamia na kumlipa mweye fedha muda ukifika.Walianza kuweka fedha mwaka 2006.
"Kimsingi fedha hizo ilikuwa ni mali ya IPTL walilipwa kupitia akaunti hiyo baada ya mgogoro kuwa umekwisha ".
Kuhusu jibu la CAG kwamba humu inawezekana zipo za umma au zipo za IPTL, "Alikuwa na maana kwamba hizi fedha tuziweke hapa, tukimaliza mzozo wetu hizi fedha chukua,"Alisema Rais.
Lakini maana nyingine ni kwamba kulikuwa na kodi za serikali ya VAT ambayo hazikulipwa, ambazo ni bilioni 21.7 baadaye TRA imepeleka madai yake kwa PAP na kwamba wamekubali kulipa kodi hiyo ya serikali.
Fedha ni za nani? hesabu 2012 CAG aliwaelekeza Tanesco alisema kuacha kuhesabu fedha za Escrow kuwa ni fedha zao.
Tarehe 5 Septemba mwaka huu Mahakama ilifanya uamuzi kwa akaunti kufungwa na PAP wakachukua fedha zao.
Kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa alisema kwamba Waziri wa Tamisemi Hawa Ghasia alisema zozezi lilienda vizuri katika halmashauri 141 na kasoro zilijitokeza katika sehemu chache, na sehemu nyingine walikamilisha jana ,Uchaguzi huu ni uthibitisho kwamba demokrasia inakwenda vizuri.
Aidha aliwapongeza walioshinda na kwamba wajipange kuwatumikia wananchi,alisema kwa mujibu wa Waziri Ghasia kulikuwa na kasoro na alichukua hatua, ikiwamo kuwafukuza kazi, kuwasimamisha, kuwashusha vyeo na kutoa maonyo kwa maofisa wazembe .
"Nampongeza kwa hatua alizochukua na nina muunga mkono na ...," Alisema kwamba watumishi wana wajibu wa kuwatumikia wananchi hasa ikitiliwa maanani kwamba wao ndiyo watakaosimamia uchaguzi mkuu ujao,na kwamba kuwawajibisha hawa ni fundisho la uchaguzi mkuu ujao.
"Kuhusu wanvunja sheria nimewaagiza wakuu wa jeshi la polisi kuwachukulia hatua wale wote waliovunja sheria, kwa kuwapeleka mahakamani, ili wasiwe na jeuri hawa," .Kuhusu tuhuma za rushwa ameagiza taarifa zipelekwe PCCB kwa uchunguzi na kwamba serikali yake inapambana na rushwa.
Kuhusu miamala katika benki ya Mkombozi, alisema kwamba serikali inashughulika na watumishi wa umma kwa mujibu wa sheria, alisema kwa watumishi wa umma hilo wanaweza kulishughulikia na lakini kwa maaskofu na masheikh hilo haliwahusu kama serikali.
Kuhusu miamala katika benki ya Mkombozi, alisema kwamba serikali inashughulika na watumishi wa umma kwa mujibu wa sheria, alisema kwa watumishi wa umma hilo wanaweza kulishughulikia na lakini kwa maaskofu na masheikh hilo haliwahusu kama serikali.
No comments:
Post a Comment