KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

December 22, 2014

SAKATA LA ESCROW: PROFESA TIBAIJUKA 'OUT'. PROF. MUHONGO AWEKWA KIPORO KWA SIKU CHACHE KUSUBIRIA UCHUNGUZI

Waziri Anna Tibaijuka
 Kuhusu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka kupokea Fedha kutoka IPTL amesema wamekaa naye naye na kuzungumza naye, "Kamati ya Maadili wanaendelea naye, mazungumzo yetu yalikuwa ni fedha za nini na amezipata kwa ajili gani, akasema amezipata kwa ajili ya shule,".
Maswali makubwa ni kwanini fedha hizi hazikwenda kwenye Bodi ya Shule na zimeenda kwenye akaunti yake, ameeleza ni masharti aliyopewa na aliyempa.
"Kuna udhaifu sana hapo wa kimaadili, kwa hiyo tumekubaliana kwamba Waziri huyu tukishazungumza naye ... tumemuomba atupe nafasi tumteue mwingine," (Shangwe na kelele zikalipuka) 
"Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo huyu tumemuweka kiporo, kuna uchunguzi nimeagiza ufanywe nitakapopata majibu nitafanya uamuzi katika siku mbili tatu zijazo ninachotaka tufanye uamuzi kwa misingi ya haki,"Alisema.


No comments:

Post a Comment