Mkurugenzi wa Lino Agency ambaye ni mmoja kati ya waandaaaji wa Miss Tanznia, Hashim Lundenga
Serikali
imelifungia shindano la Miss Tanzania kwa miaka miwili kutokana na
sababu mbalimbali na ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea, ikiwemo
udanganyifu mkubwa unaojitokeza kila mwaka kwenye shidano hilo.
Maamuzi
hayo yamechukuliwa na BASATA, ambapo Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo
Godfrey Mngereza amesema maamuzi hayo yalifikiwa baada ya kukaa kikao
cha tathmini ambapo Kamati ya Miss Tanzania ilishindwa kujibu hoja za
msingi za wadau na kukiri kuwepo udhaifu katika uendeshaji wa shindano
hilo.
“Baada
ya kupitia maelezo yote na taarifa ya tathmini ya shindano hilo ni
vyema tulisimamishe kwa muda ili mwandaaji ajipange upya, atakaporejea
arejee kwa nguvu na kuandaa shindano lenye hadhi kubwa kuliko ilivyo
hivi sasa'' alisema Mngereza.
Shindano hilo limekumbwa na kashfa mbalimbali tangu mwaka 2006 ikiwemo ya kuvisha mataji warembo wasiokidhi vigezo.
No comments:
Post a Comment