KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

December 26, 2014

UKAWA MOTO! YAWATAKA WABUNGE KUPIGA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU KUSHINIKIZA RAIS AUNDE SERIKALI MPYA !


Mwenyekiti mwenza wa vuguvugu la umoja wa katiba ya wananchi maarufu kama UKAWA, ambaye pia ni mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, (Kulia), akifafanua jambo wakati wa mkutano wa umoja huo na waandihi wa habari makao makuu ya CUF, Buguruni jijini Dar es Salaam jana. UKAWA imejibu hotuba ya Rais Jakaya Kikwete juu ya kashfa ya akaunti ya Tegeta-Escrow, kuwa hatua alizochukua hazijakidhi matarajio ya wananchi walio wengi na kutaka hatua zaidi zichukuliwe kwa kuwajibishwa wote waliotajwa.           Mwenyekiti mwenza wa Vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi, maarufu kama UKAWA, Profesa Ibrahim Haroun Lipumba, akizungumza makao makuu ya CUF, Buguruni jijini Dar es Salaam, juzi . Profesa Lipumba aliyekuwa amefuatana na viongozi wenzake wa umoja huo, James Mbatia, (NCCR-Mageuzi) na Dkt. Wilbroad Slaa, (CHADEMA), alisema, hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, aliyoitoa Jumatatu Desemba 22, 2014 na kuzungumzia kashfa ya Escrow, imezidi kuwachanganya Watanzania, ambao walitegemea Rais, angewachukulia hatua wote waliotajwa kwenye mapendekezo ya Bunge, kinyume chake amewaweka kiporo watuhumiwa wengine.Katibu Mkuu Dkt. Wilbroad Slaa
Dar es Salaam. Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umelitaka Bunge kuiwajibisha Serikali ikiwa Rais Jakaya Kikwete atashindwa kutekeleza maazimio ya Bunge ikiwamo kumng’oa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.Wakizungumza hapa jana, viongozi hao walisema endapo Rais atashindwa kumwajibisha Profesa Muhongo, basi wabunge wao watawasilisha hoja na kushawishi wengine kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu na umoja huo utaitisha maandamano nchi nzima.Mwenyekiti mwenza wa umoja huo, Profesa Ibrahim Lipumba alihoji kwa nini Rais Kikwete anasita kumwondoa Profesa Muhongo wakati Bunge lilishatoa maazimio.Alisema Bunge linalowakilisha wananchi zaidi ya milioni 45 liliazimia uteuzi huo utenguliwe lakini akaelezea kushangazwa kwake na hatua ya Rais kusema bado anachunguza.“Hivi Rais anachunguza nini, haliamini bunge? Kama anavyoteua mawaziri pia ana madaraka ya kutengua nafasi zao, sasa anasita nini wakati azimio la Bunge limemwelekeza. Kama Rais Kikwete atashindwa kumwajibisha Muhongo atakuwa ameshindwa kutekeleza moja ya maazimio ya Bunge na Ukawa utaliomba Bunge kuiwajibisha Serikali.”Alisema hotuba aliyoitoa Jumatatu wakati akiwahutubia wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, haijakidhi matarajio ya wengi kwani kuna maazimio hayajatekelezwa.Profesa Lipumba ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF, alisema Rais amekataa kutekeleza azimio la kutaka mitambo ya IPTL itaifishwe na kutoa sababu ambazo hazina mashiko.                                                                                               

No comments:

Post a Comment