Naibu Waziri wa maji Amos Makala wapili toka kulia
akimkabidhi mchezaji
bora
wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara
mwezi Novemba Rashid Mandawa wa Kagera Sugar(wapili toka kushoto) hundi
yenye thamani ya Sh. Milioni 1/=na kombe kabla ya mechi kuanza kati ya
Simba na Kagera
Sugar ambapo simba ililala kwa bao 1-0. Wengine kulia ni Makamu
Mwenyekiti wa
bodi ya ligi Said Mohamed. Kushoto Ofisa Udhamini wa Vodacom
Tanzania Ibrahim Kaude. Wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, wamekabidhi zawadi ya Sh. Milioni moja na kombe kwa mchezaji bora wa mwezi (Novemba) Rashid Mandawa wa Kagera Sugar. Zawadi hiyo ilikabidhiwa muda mfupi kabla ya kuanza kwa mechi ya raundi ya nane ya VPL ambayo Kagera Sugar waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Ijumaa. Akizungumza mara tu baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, mshambuliaji huyo wa Kagera Sugar aliwashukuru makocha, wachezaji na mashabiki wa timu hiyo kwa kumuunga mkono kwani alipata ushindani mkali kutoka kwa Fulgence Maganga wa Mgambo Shooting pamoja na Nahodha wa Simba,Mganda Joseph Owino waliofanya vizuri pia mwezi Novemba,Alisema Mandawa. "Ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kutwaa tuzo hii, ninawashukuru pia watendaji wote wa Kagera Sugar na mashabiki wetu kwa kuniunga mkono. Huu ni mwanzo mzuri kwangu msimu huu. Nitajitahidi nifanye vizuri zaidi, ikiwezekana kutwaa tuzo ya mfungaji bora. "Mpaka sasa nina magoli manne ingawa watu wengi wanajua kwamba nina mabao matatu. Nilifunga dhidi ya JKT Ruvu, Polisi Morogoro, Coastal Union na Mtibwa Sugar. Ninawaahidi mashabiki wetu kwamba sitawaangusha," alisema Mandawa. Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu alisema kampuni hiyo inajisikia fahari kwa wachezaji bora kupatikana kwani ni moja ya mafanikio ya jitihada zao na kampuni hiyo ipo tayari kuboresha maisha ya wachezaji wanaoshiriki ligi kuu ya Vodacom na maisha yao kuwa murua.Vodacom Tanzania itaendelea kuboresha ligi kuu kila mwaka na tutakuwa tunaleta ubunifu kila mwaka na tutaendelea kutoa zawadi hiyo kwa mchezaji anayefanya vizuri kila mwezi ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuongeza ushindani katika ligi hiyo alisema Nkurlu. Mandawa anakuwa mchezaji wa tatu kupewa tuzo hiyo tangu kuanzishwe utaratibu huu katika msimu huu. Kiungo Antony Matogolo wa Mbeya,. ambaye amepelekwa kwa mkopo Panone FC ya Kilimanjaro, alikuwa mchezaji wa kwanza kupewa tuzo hiyo kama mchezaji bora wa Mwezi Septemba kabla ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Salum Abubakar 'Sure Boy' kuibuka mchezaji bora wa Oktoba. Kikosi cha Kagera Sugar kilikosa huduma ya Mandawa katika mchezo uliopita dhidi ya Simba kwa sababu iliyoelezwa na Kocha Mkuu wa wakata miwa hao wa Kagera, Maganda Jackson Mayanja kuwa alikuwa anasumbuliwa na majeraha ya kifundo cha mguu (enka) wa kushoto. Wachezaji wengine wenye mabao manne sawa na Mandawa kabla ya mechi za VPL mwishoni mwa wiki ni Mrundi Didier Kavumbagu wa Azam FC, Mkenya Rama Salim wa Coastal Union, Ame Ally Amour wa Mtibwa Sugar na Dan Mrwanda (Polisi Morogoro/Yanga). |
December 27, 2014
WADHAMINI WAKUU WA LIGI KUU YA VODACOM WAMZAWADIA MANDAWA WA KAGERA SUKARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment