Washindi wa shindano la AppStar wakionyesha zawadi zao za pesa taslimu walizokabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Abigail Ambweni (wa tatu toka kushoto) Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo mwishoni mwa wiki. Shindano hilo linaendeshwa na kampuni hiyo. |
Mshindi wa kwanza wa shindano la AppStar tabaka la wabunifu waliobobea Roman Mbwasi akielezea jambo wakati wa shughuli ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao iliyofanyika makao makuu ya Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki hii. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Abigail Ambweni, akimsikiliza kwa makini pamoja na mshindi wa kwanza katika tabaka la wabunifu chipukizi, George Machibya (kulia) Shindano hilo linaendeshwa na kampuni hiyo. |
Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Abigail Ambweni (kushoto)
akimkabidhi zawadi ya pesa taslimu Tsh. milioni 2/- mshindi wa kwanza wa
shindano la AppStar tabaka la wabunifu
waliobobea ambao programu zao tayari zinatumiwa na watu zaidi ya 50,000
Roman Mbwasi (wa pili toka kushoto). Shindano hilo linaendeshwa na
kampuni hiyo.
Dar es Salaam, Sunday December 21, 2014: Washindi 4 wa shindano la kubuni programu za simu
lililoandaliwa
na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania lijulikanalo kama
AppStar leo wamekabidhiwa zawadi zao ikiwa ni fedha taslimu na washindi
wawili kati yao watashiriki
katika kinyang’anyiro cha shindano hilo ngazi ya kimataifa
litakalofanyika Bangalore nchini India Januari 15,2015.
Waliokabidhiwa
zawadi ni Roman Mbwasi ambaye amejinyakulia shilingi milioni mbili na
atagharimiwa safari ya kwenda
nchini India kushiriki shindano hili ngazi ya kimataifa akiwa ni
mshindi wa kwanza katika kundi la wabunifu wakongwe na Athumani Mahiza
alinyakua shilingi milioni moja; yeye ni mshindi wa pili.
Katika
kundi la wabunifu chipukizi George Machibya ndiye mshindi wa kwanza
aliyejinyakulia shilingi milioni moja na
atagharimiwa safari ya kushiriki katika ngazi ya kimataifa nchini India
na Ilakoze Jumanne amefanikiwa kujinyakulia shilingi laki tano akiwa ni
mshindi wa pili.
Akiongea
wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo,Meneja wa Uhusiano wa Masuala
ya Nje wa Vodacom Abigail Ambweni alisema
Vodacom inawapongeza washindi na wote waliojitokeza kushiriki katika
shindano hili muhimu linalolenga kuibua na kukuza vipaji vya
Watanzania.
“Tukiwa
tunaongoza katika kutoa huduma za mawasiliano kwa njia ya teknolojia,
Vodacom ina jukumu la kukuza sekta hii na
kuibua vipaji vya matumizi ya teknolojia ili ziwepo programu mbalimbali
za kurahisisha maisha kwa watumiaji wa simu. Tutazidi kuboresha
shindano hili siku za usoni ili liweze kuhusisha Watanzania wengi
hususani vijana waliopo vyuoni na nia yetu ni kukuza ubunifu
wa kiteknolojia hapa nchini,” alisema Ambweni.
Nao
washindi wa shindano hilo walishukuru Vodacom kwa kuwazawadia na
kuandaa shindano hili kwa kuwa linawawezesha
Watanzania kuchemsha bongo zao kubuni programu zenye kuleta suluhisho
katika kupambana na changamoto mbalimbali na kurahisisha maisha.
Roman Mbwasi amesema kuwa shindano hili linasaidia kuwafanya watanzania wawe wabunifu na aliongeza kuwa ana uhakika
atafanya vizuri katika ngazi ya kimataifa kupitia program yake aliyoibuni ya upashanaji wa taarifa za barabarani.
Naye
George Machibya alisema kuwa wakati umefika kwa Watanzania kuchangamkia
fursa kama hizi kwa kuwa nchi bado inahitaji
kuwa na wabunifu wa program mbalimbali za kurahisisha maisha badala ya
kutegemea program za nje ambako mazingira ya kule na ya kwetu ni
tofauti. “Nina uhakika wazo la program yangu ya Soko Huru litafanya
vizuri katika ngazi ya kimataifa na fursa hii imenifanya
nizidi kujiamini zaidi,” alisema.
Mshindi
atakayepatikana katika kinyang’iro cha awamu ya pili atashiriki
katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Mitandao
ya Simu za Mkononi utakaofanyika Barcelona nchini Hispania. Mashindano
ya mwaka huu yanawashirikisha washiriki kutoka nchi za Afrika ya Kusini,
Misri Tanzania, Kenya, Ghana na India.
|
No comments:
Post a Comment