Mbunge
wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ,wa kwanza kushoto akikabidhiwa
dhana za kimila na wazee wa Kijiji cha Msoga pamoja na kukaribishwa
rasmi na wazee hao kijiji hapo juzi.(Picha zote na Mwamvua Mwinyi .
…………………………………………………………………………..
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
Wazee wa kijiji cha Msoga,katika
kata ya Msoga ,Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani ,wamemkabidhi
zana za jadi mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ikiwa ni moja
ya ishara ya kumpokea kijijini hapo rasmi..
Wazee hao walifanya shughuli hiyo mapema juzi na kumtaka mbunge huyo kuendelea umoja na mshikamano nadani ya jimbo hilo.
Nae Ridhiwani Kikwete
akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zana hizo amewashukuru wazee hao
na kuahidi kutekeleza masuala ya maendeleo ili jimbo hilo liweze kutoka
katika hatua iliyopo sasa.
Aidha Ridhiwani amesema suala la
mila na desturi linatakiwa lidumishwe pasipo kulipa kisogo kwa faida ya
vizazi vya sasa na baadae .
KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA ATEMBELEA KITUO CHA AFYA MSOGA
Mbunge wa jimbo la Chalinze,Bagamoyo mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete wa kwanza kulia alipoitembelea kituo cha afya cha Msoga juzi ,ambacho kinakaribia kukamilika(Picha zote na Mwamvua Mwinyi)
Kituo cha afya cha Msoga,kata ya Msoga ,Chalinze ,Bagamoyo Mmkoani Pwani,kikionekana kikiwa katika hatua za mwisho kukamilika kwa ujenzi wake ulioanza mwaka jana,ambapo hadi kukamilika kwake kitagharimu zaidi ya sh.mil 500
No comments:
Post a Comment