BUNGE
limepitisha rasmi Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya wa mwaka
2014, huku adhabu ya kifo kwa watakaokutwa na dawa hizo, ikishindikana
kuingizwa kwenye muswada huo, isipokuwa mapapa na vigogo wa biashara hiyo,
wameongezewa adhabu ya faini ya Sh bilioni moja na kifungo cha maisha. Hata
hivyo, baadhi ya wabunge bado wameendelea kung’ang’ania kuwa sheria hiyo
ijumuishe adhabu hiyo kali ya kifo kwa wafanyabiashara, mapapa au vigogo
wanofadhili biashara hiyo, kwa kuwa madhara ya dawa hizo ni makubwa na
yanaathiri zaidi vijana ambao ni nguvukazi ya nchi.Akitoa majumuisho ya
michango ya wabunge kuhusu hoja ya muswada huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama, alisema adhabu ya kifo
haiwezekani kuingizwa kwenye sheria hiyo, kwa kuwa adhabu hiyo nchini iko
kwenye makosa mawili pekee.“Ni kweli Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo bado
zinatoa adhabu ya kifo, lakini kwa mujibu wa sera iliyopo, adhabu ya kifo
imeingizwa na kubainishwa kwenye makosa ya uhaini na mauaji pekee,” alisema
Mhagama.
No comments:
Post a Comment