Mh.Lowassa |
SIKU moja baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kumuonya
aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, kwa tuhuma za kukiuka Katiba na kuanza
kampeni za Urais kabla ya muda, kiongozi huyo ameibuka na kudai kuwa hana njia
ya kuwazuia watu wasimuombe agombee Urais.
Pia Lowassa ametumia nafasi hiyo na kuwaomba wale wote ambao
bado wana nia ya kumshawishi agombee nafasi hiyo ya urais, wasubiri kwanza hadi
pale chama chake hicho kitakapotoa maelekezo.Akizungumza na vijana 60 wa
bodaboda kutoka wilaya ya Mbarali, Mbeya waliokwenda pia kumshawishi agombee
nafasi hiyo, mjini Dodoma jana, alisema si vyema kwa maofisa wa chama
kuzungumzia masuala ya wanachama wao kwenye vyombo vya habari wakati kuna vikao
vya chama.
Alisema watu waliojitokeza na kumshawishi kuchukua fomu za
kuwania nafasi hiyo ya Urais, hajawaita wala kuwalipa chochote kama inavyodaiwa
na kwamba walikuwa wakifuata maneno ya Rais Jakaya Kikwete aliyoyatoa mkoani
Ruvuma katika sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya Uhuru.Alisema katika siku
hiyo, Rais Kikwete aliwataka watanzania wawashawishi viongozi wanaoona wanafaa
ili wajitokeze kugombea nafasi hiyo ya Urais.
“Mimi ni vigumu kuzuia mafuriko kwa mikono. Nazuia mafuriko
kwa mikono, yanakuja mimi nayazuia kwa mikono, nitaweza kweli? Hawa watu sina
hoja nao, sina cha kuwaambia,” alisema Lowasa.Alisema tangu makundi hayo yaanze
kujitokeza kumshawishi kuchukua fomu mambo mengi ya ajabu yamesemwa jambo
ambalo linamsikitisha na kumshangaza kwa kuwa endapo kuna mtu wa chama mwenye
hoja, ni vyema kuwasilisha kwenye vikao vya chama badala ya kuzungumza
hadharani na kwenye vyombo vya habari.HABARI LEO
No comments:
Post a Comment