Rais
Jakaya Kikwete amekabidhiwa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali (CAG) ya mwaka unaoishia Juni 2014 na kuagiza vyombo vya
dola kuwabaini maofisa wote wa Serikali wanaohusishwa na matumizi mabaya
ya fedha za umma, ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Pia, Rais
Kikwete ameagiza kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa maofisa
wote wa Serikali ambao wanahusika katika kulipa mishahara hewa kwa
watumishi ambao wameacha kazi, wamefariki dunia au wamestaafu lakini
wanaendelea kulipwa kupitia akaunti zao za benki.
Rais
ametoa maagizo hayo jana baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo na CAG Profesa
Mussa Assad. Aliiomba ofisi hiyo kuisaidia Serikali kuboresha mfumo wa
zabuni kwani Serikali inapoteza fedha nyingi kwa kupitia mchakato mrefu
wa kupatikana kwa wazabuni wa kutoa vifaa na huduma kwa Serikali
No comments:
Post a Comment