Taifa
lenye wakaazi wengi barani Afrika, Nigeria, leo linapiga kura kumchagua rais mpya, katika uchaguzi ambao una
mvutano mkubwa kuwahi kuonekana tangu nchi hiyo kupata uhuru.
Wagombea wakuu katika uchaguzi wa Nigeria, Mohammadu Buhari na Goodluck Jonathan(kulia)
Kuanzia
mji mkubwa kabisa wa Lagos katika eneo la Wakristo upande wa kusini mwa
nchi hiyo hadi katika miji upande wa kaskazini ambako kunapatikana
Waislamu wengi, vituo vya kupigia kura vilitarajiwa kufunguliwa mapema
asubuhi, ambapo kiasi ya Wanigeria milioni 68.8 kati ya wakaazi milioni
173 wamejiandikisha kupiga kura.
Rais
Goodluck Jonathan amewasili kwa helikopta katika mji alikozaliwa wa
Utuoke kusini mwa jimbo la Bayelsa usiku wa jana Ijumaa, kwa matumaini
ya kupata muhula wa pili wa uongozi licha ya ukosoaji mkubwa katika
rekodi yake.
Mpizani
wake mkubwa , mtu aliyejitangaza kupambana na ufisadi katika serikali
Muhammadu Buhari , alikuwa mjini Daura, katika jimbo la kaskazini la
Katsina, akilenga kurejea kwa njia ya kidemokrasia madarakani baada ya
kuwapo madarakani kwa muda kama mtawala wa kijeshi katika miaka ya 1980
No comments:
Post a Comment